Home Habari za michezo MWARAMU NA WENZAKE KUNZA KUANIKA UKWELI WOTE MAHAKAMANI…

MWARAMU NA WENZAKE KUNZA KUANIKA UKWELI WOTE MAHAKAMANI…

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzuia Dawa za kulevya (DCEA), Gerald Kusaya amesema leo Jumatatu Novemba 21.2022 baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya akiwemo, kocha wa makipa wa timu ya Simba, Muharami Sultan (40) na mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi Seif watafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Zikiwa zimepita siku sita tangu DCEA alipotangazwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao Novemba 15, 2022 hii leo watapandisahwa kwaajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Mbali na Muharami Sultani anayedaiwa kukutwa na kilo 34.89 za dawa za kulevya aina ya heroin na biskuti 50 zilizotengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya aina ya bangi, wengine waliotajwa ni pamoja na mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zuberi seif, Said Matwiko mkazi Magole.

SOMA NA HII  SAKATA LA MANARA GSM WATAJWA,KUNA MBUKINAFASO WA YANGA,NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here