Home Habari za michezo RASMI: PETER BANDA NNJE YA UWANJA MPAKA MWAKANI…

RASMI: PETER BANDA NNJE YA UWANJA MPAKA MWAKANI…

Habari za Simba

Afisa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema watamkosa mchezaji wao Peter Banda kwa miezi miwili kutokana na kupata majeraha katika mchezo wao wa NBCPL waliocheza dhidi ya Singida Big Star Fc mkoani Singida.

“Mchezo wetu uliopita pale Singida, mchezaji wetu Peter banda alitolewa nje baada ya kupata majeraha na uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa angeweza kukaa nje kwa wiki nne, lakini leo (jana) uchunguzi wa kina umefafanyika na imbeainika atakaa nje kwa zaidi ya miezi miwili.

“Makadirio ni kwamba Peter Banda atarejea uwanjani mwezi Februari wakati michuano ya Kimataifa hatua ya makundi itakapoanza. Kwa hiyo Wanasimba watambue hilo,” amesema Ahmed Ally.

SOMA NA HII  JERRY MURO:- "MANARA SIO MWANAYANGA....HASIRA ZIKIMWISHA ATARUDI ALIKOTOKA..."

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here