Home Habari za michezo RONALDO : ROONEY ANAWIVU …NIMEMZIDI MPAKA MUONEKANO…

RONALDO : ROONEY ANAWIVU …NIMEMZIDI MPAKA MUONEKANO…

Mshambuliaji wa Manchester United, Christiano Ronaldo amefunguka juu ya ukosoaji wa Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney hivi karibuni.

“Sijui kwa nini ananikosoa sana… pengine kwa sababu yeye wakati wake umekwisha huku nikiwa bado naendelea kucheza soka la kulipwa. Tulianza pamoja sio hivyo tu hata muonekano nimemzidi kwa sasa”

Ronaldo na Rooney ambao wote wana umri wa miaka 37 huku Mreno huyo akimzidi Rooney kiumri kwa miezi walikuwa na wakati mzuri pamoja kama washambuliaji pacha kati ya 2004 na 2009.

Magoli yao yaliisaidia Manchester United kutwaa Mataji ya Ligi mfululizo na Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini uhusiano wao huo haukumzuia Rooney kumbwatukia Ronaldo juu ya mwenendo wa tabia yake hivi karibuni kukataa kucheza dhidi ya Tottenham.

Awali Rooney aliwasihi Mashetani hao Wekundu kumuuza Ronaldo kabla ya kudai kuwa Ronaldo wa sasa sio yule wa zamani.

SOMA NA HII  'MZIMWI' WA SONSO WAITESA RUVU SHOOTING...MKWASA AVUNJA UKIMYA..AFUNGUKA HALI ILIVYO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here