Home Habari za michezo SIMBA KUMEKUCHWA…MAKOCHA WAWILI KUTUA…STRAIKA LA MABAO KUTOKA GHANA LATAJWA…

SIMBA KUMEKUCHWA…MAKOCHA WAWILI KUTUA…STRAIKA LA MABAO KUTOKA GHANA LATAJWA…

Baada ya kikosi cha Simba kuwa na wachezaji wengi majeruhi, mabosi wa timu hiyo wapo kwenye hatua za mwisho kumshusha nchini kocha mpya wa viungo atakayekuja kuchukua nafasi ya Karim Sbai aliyeondoka pamoja na kocha, Zoran Maki.

Taarifa kutoka ndani zinaeleza mabosi wa Simba wameanza harakati za kuboresha benchi la ufundi na kulipa nguvu za wataalamu wapya pamoja na kuwafuatilia wachezaji wapya ambao watawasajili kwenye dirisha dogo akiwemo mshambuliaji raia wa Ghana, Kwame Opoku.

Maboresho ya kwanza kuna mtaalamu na kocha wa viungo aliyekuwa akifundisha kwenye nchi za Kiarabu na kabla ya wiki hii kumalizika atatambulishwa na kuanza kazi hiyo.

Inaelezwa kuwa mtaalamu wa kuchua misuli ndani ya Simba, Msauzi Fareed Casssiem ndiye aliyempendekeza kocha huyo wa viungo na kuwahakikishia mabosi zake pamoja na kocha mkuu, Juma Mgunda atakuja kuongeza nguvu kulingana na mahitaji ya msingi ya wakati huu.

Simba haina kocha wa makipa tangu alivyoondoka Mohamed Rachid raia wa Morocco aliyekuwa akifanya kazi pamoja na Zoran aliyetimkia Misri.

Katika mechi mbili za Simba dhidi ya Singida Big Stars na Ihefu wakati wa kupasha misuli moto makipa, Aishi Manula na Benno Kakolanya walikuwa wanafanyishwa mazoezi na mwenzao chaguo la tatu, Ally Salim aliyekuwa anafanya majukumu ya kocha wa makipa.

Baada ya maboresho hayo mawili, mabosi wa Simba watafanya kikao kingine kizito cha uamuzi wakati kocha Selemani Matola yupo kwenye masomo ya ukocha wa lesini A ya CAF na Mgunda akitafutiwa kocha mwingine wa kusaidiana nae.

Alipotafutwa Mgunda alisema suala la kuletewa kocha wa viungo kutokana na uwepo wa wachezaji wengi majeruhi mfululizo hilo tayari amewasiliana na mabosi zake na wamemueleza siku si nyingi linakamilika.

SOMA NA HII  KUHUSU MAMELOD SUNDOWNS KUMTAKA MAYELE...UKWELI WOTE HUU HAPA...YANGA HAWAWEZI KUCHOMOA HAPA...