Home Azam FC TETESI:BAKHRESA KUPELEKA MAUMIVU YANGA….FEI TOTO NI SUALA LA MUDA TU KUTUA AZAM...

TETESI:BAKHRESA KUPELEKA MAUMIVU YANGA….FEI TOTO NI SUALA LA MUDA TU KUTUA AZAM FC..

Ikiwa imesalia takribani miezi miwili dirisha Dogo la usajili la mwezi Januari kufunguliwa, inasemekana Bosi wa Azam FC, Yusuf Bakhresa ameanza kufanya michakato ya kuboresha kikosi cha Azam na rada yake imetua kwa Nyota wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto).

Inasemekana Fei Toto na Bakhresa wapo mezani kujadili matakwa ya mchezaji huyo na endapo wataafikiana basi kiungo huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini akiwa na kikosi cha Yanga huenda akamwaga wino kuwatumikia matajiri wa Jiji la Dar es Salaam.

Fei Toto ana Mkataba na mabingwa hao watetezi hadi mwaka 2024 na inasemeka kuwa kuvunja mkataba wake anahitajika kuwalipa Yanga Tsh. milioni 100 na mshahara wake wa miezi mitatu.

SOMA NA HII  DILI LA AJIB KURUDI ZAKE YANGA LIMEFIKA HATUA HII..