Home Habari za michezo YANGA MPOO….?…NABI ATAKA MAMBO KAMA YA SIMBA HUKO….PLUIJM APIGWA NA BUTWAA…

YANGA MPOO….?…NABI ATAKA MAMBO KAMA YA SIMBA HUKO….PLUIJM APIGWA NA BUTWAA…

Habari za Yanga SC

Baada ya kuiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji, kocha wa kikosi hicho Nasreddine Nabi ameanza kuipigia hesabu Mbeya City, huku akiamini vijana wake wanaweza kuwafanya Wananchi wafurahie mataji mfululizo ‘back to back’ kama za Simba miaka minne iliyopita na sio rekodi pekee.

Ushindi wa juzi, Jumanne kwenye Uwanja wa Liti dhidi wa wenyeji, Dodoma Jiji umemfanya Nabi kuiongoza Yanga michezo 48 ya Ligi Kuu Bara bila ya kupoteza, jambo ambalo halijawahi kutokea nchini.

Nabi ambaye mara baada ya mchezo huo na kikosi chake walianza safari ya kurejea Dar kupitia Dodoma, alisema shauku yake ni kuona mashabiki wa Yanga wakifurahia mataji na ndio maana amekuwa akiumiza kichwa kusuka kikosi ambacho hakuna timu ambayo itamudu kushindana nacho.

“Inawezekana kutwaa mataji mfululizo, lakini jambo muhimu ni kuwa pamoja. Tunatakiwa kuwa na njaa kwa kufanya vizuri kwenye kila mchezo bila kuangalia nini ambacho wapinzani wetu wanafanya. Tukiangalia nyuma tunaweza kupoteza mwelekeo,” alisema Nabi.

Kwa sasa anasema ni mapema kuzungumzia ubingwa, lakini anatamani kuona mashabiki wa timu hiyo wakifurahia zaidi mataji maana kuwa na rekodi nzuri ya kutopoteza kisha wakishindwa kuchukua kubingwa ni kazi bure.

Nabi ambaye ameivusha Yanga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, anaonekana kuguswa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na mapenzi makubwa waliyonayo kwake.

“Nguvu ya shabiki ni kubwa. Wamekuwa pamoja nasi katika nyakati zote. Naamini kuwa wataendelea kutuunga mkono. Tunarudi nyumbani na tuna mchezo mgumu mbele yetu,” alisema kocha huyo raia wa Tunisia.

Mara baada ya Yanga kucheza dhidi ya Mbeya City yenye mshambuliaji hatari, Sixtus Sabilo mwenye mabao sita na asisti tano, itakwenda Mbeya kucheza dhidi ya Ihefu, Novemba 29.

Leo Yanga itakuwa ikisaka rekodi ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England kwa kucheza michezo 49 bila kupoteza ambayo washika mitutu hao wa London waliiweka kuanzia Mei 7, 2003 hadi Oktoba 16, 2004.

YAMSHTUA PLUIJM

Katika hatua nyingine kiwango cha Yanga kimemstua kocha wa Singida Big Stars, Hans van der Pluijm ambaye anaamini kuwa ana kazi kubwa ya kufanya na vijana wake ambao asilimia kubwa ni wapya kikosini ili kuwa bora zaidi.

SOMA NA HII  MCHAMBUZI: SIMBA IMEBEBWA NA YANGA KIMATAIFA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here