Home Azam FC AZAM: ‘UNBEATEN’ YA YANGA ILILINDWA SANA NA WAAMUZI…

AZAM: ‘UNBEATEN’ YA YANGA ILILINDWA SANA NA WAAMUZI…

Msemaji wa klabu ya Azam Fc Thabit Zakaria maarufu kama Zakazakazi amesema kua rekodi ya kutokufungwa kwa klabu ya Yanga imelindwa na waamuzi kwa muda mrefu.

Zakazakazi anaamini klabu ya Yanga ilipaswa iwe imeshafungwa kwa muda mrefu ila kutokana tu na ubovu wa waamuzi wetu kwenye kutoa maamuzi imeifanya klabu hiyo kutokufungwa muda mrefu mpaka kufikisha michezo 49.

Zakazakazi pia alipigilia msumari kwa kusema kudhihirisha hilo licha ya Yanga kufungwa leo lakini pia lao kwenye mchezo huo lililofungwa na Yannick Bangala mchezaji huyo alikua ameotea na bao hilo kwa mujibu wa kanuni sio bao halali, Lakini kutokana na makosa ya waamuzi limekua bao na kuwapa faida Yanga.

Klabu ya Yanga juzi imehitimishiwa rekodi ya kutokufungwa kwenye michezo 49 ya ligi kuu ya NBC baada ya kukubali kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya klabu ya Ihefu kutoka Mkoani Mbeya katika mchezo uliopigwa katika dimba la Highland state

SOMA NA HII  SIMBA WAFUNGUKA... ISHU YA KUINGIZA MASHABIKI BURE KWA MKAPA...MECHI DHIDI YA HOROYA..