Home Azam FC AZAM WAPANIA KWA FEI TOTO…WAMWEKEA MIL 350 MEZANI PAMOJA NA MSHAHARA WA...

AZAM WAPANIA KWA FEI TOTO…WAMWEKEA MIL 350 MEZANI PAMOJA NA MSHAHARA WA MIL 10 KWA MWEZI..

Fei toto Yanga SC

Kiungo wa Yanga SC, Feisal Salum (Fei Toto) huenda akatimkia kunako klabu ya Azam mwisho mwa msimu huu (2022/23) baada ya Azam kumuwekea mezani takribani Tsh. Milioni 350 kama pesa ya usajili.

Katika kuhakikisha wanainasa saini ya kiungo huyo Azam wapo tayari kutanguliza kishika uchumba ambapo kila mwezi Fei Toto atapokea Milioni 10 hadi dirisha kubwa la usajili litakapo funguliwa na kumwaga wino rasmi kuwatumikia matajiri hao wa jiji la Dar es Salaam.

Inasemekana Azam wamekubali kuuvunja mkataba wa Fei na Yanga ambapo watalipa milioni 100 na mshahara wa miezi mitatu kama masharti yaliyopo kwenye mkataba wake na Yanga.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO...SIMBA NAO HAWAKO KINYONGEE AISEE...WAPANGA KUZIFUATA AL AHLY NA ZAMALEKI MISRI...