Home Habari za michezo KIGWANGALA: KAMA MO DEWJI AMESHINDWA SIMBA AWEKE WAZI…NIKO TAYARI KUTAFUTA NAMNA…

KIGWANGALA: KAMA MO DEWJI AMESHINDWA SIMBA AWEKE WAZI…NIKO TAYARI KUTAFUTA NAMNA…

Kigwangalla na Mo dewji

Mbunge wa Nzega Vijijini na mwanachama wa Klabu ya Simba SC na Dk Hamisi Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram ameandika

”Sijui kuna kitu gani kinaendelea ndani ya klabu yetu ya Simba. Sijui kwa uhakika, lakini nasoma comments za wadau/washabiki wa Simba kwenye kurasa zangu za mitandao ya kijamii na wengine wakichukua muda wao kuniandikia meseji kabisa.”

”Baadhi wakitaka nigombee uongozi ndani ya Simba, na wengine wakinisimanga kuwa ninunue hisa za Simba sasa kwa kuwa tajiri anauza hisa zake!”

”Kuhusu kugombea nafasi yoyote ile ya uongozi ndani ya Simba, jibu langu mara zote limekuwa HAPANA! Kiukweli, sijawahi kutamani kuwa kiongozi wa Simba hata mara moja. Mimi ni mshabiki na mwanachama tu. Itabaki kuwa hivyo.”

”Kitu cha wengi lazima kiwe na maneno tu, sababu ni cha wengi. Usitegemee watu watanyamaza. Wabunge tunasemwa kila siku, why? Sababu ni mali ya umma, tumetaka wenyewe. Hata muwekezaji wetu angetaka asisemwe angeanzisha klabu yake kama Mzee Bakhresa tu, wala asingetusikia kumsema.”

”Ukitaka kuchukua hisa za klabu kama Simba ni lazima uwe mkweli, muwazi na serious kidogo. Ukileta janja janja tutakuvumilia kidogo mwisho tutasema. Klabu yetu ina maslahi ya umma na ni lazima tutayalinda siku zote. Kama siyo Kilomoni, basi ni Kigwangalla, ama Kingwendu.”

”Kama kweli muwekezaji ameshindwa kuwekeza, na anataka kuondoka, menejimenti ya Simba waweke wazi, wanasimba tutaamua. Siyo kuleta vijembe.”

”Mimi sijawahi kufikiria kuwekeza kwenye mpira lakini nikilazimika kufanya hivyo, niko tayari kufikiria na kutafuta namna.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA JUMAPILI...RALLY BWALYA AFUNGUKA HAYA DHIDI YA WAZAMBIA WENZAKE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here