Home Habari za michezo NABI : HAWA SIMBA WATAANZA KUSHINDA MECHI ZAO KWA KASI…

NABI : HAWA SIMBA WATAANZA KUSHINDA MECHI ZAO KWA KASI…

Habari za Yanga SC

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga juzi jioni walikiwasha na Ihefu kwenye Uwanja wa Mbarali, Mbeya na matokeo kama ulivyoyaona.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amesisitiza kwamba huu ndiyo muda wa kukusanya pointi za ubingwa kwani kwenye mzunguko wa pili upepo utabadilika.

Kocha huyo anayesaka rekodi ya kipekee na Yanga msimu huu ametabiri kwamba Simba watakuja na nguvu ya hatari kwenye mzunguko wa pili na wanaweza kubadili upepo kabisa.

“Shika haya maneno yangu hii Simba itarudi kwa nguvu kubwa zaidi kwenye michezo ya mzunguko wa pili ili kupunguza umbali wa pointi tuliyoacha, kwetu tunalifahamu hilo na tumejipanga wachezaji na benchi la ufundi kuendelea kubaki kileleni mwa ligi hadi mwisho wa msimu na hilo linawezekana,” alisema Nabi.

“Hawa wenzetu Simba na Azam ambao ukiangalia kwa makini tupo nao kwenye mbio za ubingwa wa ligi wataimarika zaidi ili kuendekea kubaki kwenye nafasi za juu na kupunguza umbali wa pointi tulizowaacha.

“Ukiangalia Azam wamerudi kwenye mbio za ubingwa embu angalia timu yao ilivyoimarika wakati huu imeshinda mechi saba mfululizo kiwango cha juu kabisa imeonyesha kwahiyo wenyewe wametambua ubingwa unatafutwa wakati huu na si badae,”alisema Nabi ambaye ameanza mikakati ya dirisha dogo.

Nabi alisema ligi ilivyo wakati huu hakuna muda wa kufanya maandalizi ya kutosha kutoka mechi moja kwenda nyingine kwani ratiba inaonyesha kila baada ya siku tatu kila timu inatakuwa kucheza na ndio muda ambao mtu ukiwa mjanja unavuna pointi.

Aliwapongeza wachezaji wake kwa kufanya kila anachowaelekeza hata mechi zilizokuwa ngumu kutokana na kuchoka kwao kwa kukosa muda mzuri wa kupumzika na kufanya maandalizi bado wanapata ushindi.

“Ukiangalia timu nyingine 15, zilizopo kwenye ligi hakuna inayoweza kucheza kwenye mazingira kama yetu na bado ikaendelea kupata matokeo bora, wakati mwingine kuna baadhi ya wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kwanza tunawakosa ila bado tunapata ushindi,” alisema Nabi na kuongeza;

“Ukiangalia kuna mechi hatuna, Diarra, Yannick Bangala, Azizi Ki, Djuma Shaban, Benard Morrison na wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza na bado tunashinda licha ya wakati mwingine kushindwa kucheza vizuri kama ile mechi ya Kagera Sugar,”

“Tunafanya mabadiliko wa wachezaji wale wanaopata nafasi wanaenda kutimiza majukumu yao na kupata matokeo mazuri kwa upande wetu lakini hali kama hii uipeleke kwenye timu nyingine ya kutoa wachezaji watano wa kikosi cha kwanza sidhani kama zinaweza kufanya vizuri,

“Kwa nini ubingwa unatafutwa sasa…?, nakuambia kwenye mzunguko wa pilj hata hizi timu zilizofanya vibaya kwenye mzunguko wa kwanza hazitakuwa wanyonge tena kwani zinahitaji kushinda kila mchezo ili kusalia kwenye ligi,”

“Kwenye mzunguko wa pili kila timu itafanya usajili ili kuongeza makali ya kikosi chao na kupunguza au kuondoa madhaifu ya nzunguko wa kwanza kwahiyo ugumu wa ligi utaongezeka kwenye kila mechi.

SOMA NA HII  YANGA WALIVYOPOKELEWA KIFALME MWANZA LEO...GEITA GOLD YAWAHI KUFANYA YAO KIRUMBA MAPEEMAA...