Home Habari za michezo TETESI….THOMAS ULIMWENGU NI SIMBA AU YANGA…DILI LAKE LIKO HIVI…

TETESI….THOMAS ULIMWENGU NI SIMBA AU YANGA…DILI LAKE LIKO HIVI…

Habari za Yanga

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa rasmi jana Desemba 15 huku mshambuliaji Thomas Ulimwengu aliyekuwa akikipiga TP Mazembe yupo nchini na anasikilizia dirisha hili atue wapi baada ya mkataba wake na Mazembe kumalizika rasmi Julai 1, 2022.

Mmoja wa rafiki wa karibu wa mchezaji huyo alisema kama utatumika ushawishi mkubwa kwa mchezaji huyo anaweza kufikiria kucheza nchini kutokana na soka linavyokuwa kwa kasi sasa.

“Ulimwengu kweli yupo nchini lakini hapendi kuonekana, yeye anajifungia kivyake na hajafikiria kwa sasa kucheza nyumbani lakini inawezekana akakubali kama ushawishi mkubwa utatumika,” kilisema chanzo hicho.

Katika dirisha hili, timu za ligi kuu zinataka kuimarisha vikosi vyao, zikiwamo Simba na Yanga zinazohaha kusajili nyota wenye uzoefu watakaozisaidia hasa kwenye michuano ya CAF.

Simba inahaha kutafuta mshambuliaji ambaye ataenda kusimama kwenye eneo la ushambuliaji baada ya sasa kulazimika kumtumia Moses Phiri kama mshambuliaji wa kati huku namba yake halisi ikiwa ni mshambuliaji wa pembeni.

Upande wa Yanga pindi anapokosekana Fiston Mayele basi huwa wanahaha lakini mabosi wa klabu hiyo wameweka wazi watavunja kibubu ili kupata mshambuliaji ambaye atawasaidia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Awali Ulimwengu aliwahi kuhitajika na Simba na Yanga huku ikidaiwa mabosi wa Simba walikuwa wamempandia dau zuri lakini mchezaji huyo alipopokea ofa ya kurudi tena TP Mazembe aliamua kusepa zake na alisaini miaka miwili 2020-2022.

SOMA NA HII  GEITA GOLD WANOGEWA NA DUCHU...MIKAKATI YAFANYWA KIMYA KIMYA KUEPUSHA SHARI ZA SIMBA NA YANGA...