Home Habari za michezo WAARABU WAMFANYIA KUFRU RONALDO…KULIPWA MSHAHARA BIL 40 KWA MWEZI…

WAARABU WAMFANYIA KUFRU RONALDO…KULIPWA MSHAHARA BIL 40 KWA MWEZI…

Cristiano Ronaldo amekubali dili la TZS bilioni 494 kwa msimu na Al-Nassr FC ya Saudi Arabia sawa na Bilioni 40 kwa mwezi.

Ronaldo ambaye ni mchezaji huru anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo Januari 2023 kwa mkataba wa miaka miwili na nusu, hivyo kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa ghali zaidi duniani.

Hivi karibuni, Ronaldo aliingia kwenye mvutano na kocha wake Ten Hag wa Man U ambapo Ronaldo aliwasema vibaya Man U kwenye mahojiano yake ambayo yalizua gumzo na mwishoni uongozi wa timu hiyo ulimalizana naye kwa makubaliano ya pande zote mbili.

SOMA NA HII  GWARIDE LA UBINGWA YANGA LAWA GUMZO AFRIKA...MITANDAO MIKUBWA YALIPA UZITO...WAARABU WAPAGAWA...