Home Habari za michezo YANGA PRINCESS WAMFUTA MAYELE KUWAPA UJANJA WA KUITUNGUA SIMBA QUEENS..

YANGA PRINCESS WAMFUTA MAYELE KUWAPA UJANJA WA KUITUNGUA SIMBA QUEENS..

Desemba 22, 2022, mwaka huu ni ‘Derby ya Kariakoo’ kwa upande wa soka la wanawake. Timu  ya Yanga Princess itacheza dhidi ya Simba Queens.

Yanga Princess wataingia kwenye mchezo huo wa tatu wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu, wakitoka kuifumua Mkwawa Queens mabao 4-0.

Akizungumza, Mratibu wa kikosi hiko, Kibwana Matokeo amesema kikosi hiko kitafanya mazoezi yake mchana leo kwenye uwanja wa Avic, uliopo Kimbiji, Dar Es Salaam.

”Uwanja huo unatumiwa pia na timu kubwa ya Wanaume kwenye mazoezi yao na mechi za kirafiki na Kibwana anaamini kitendo cha Princess kufanya mazoezi hapo kitawakengenea kujiamini sana kuelekea mchezo wa Derby” amesema Kibwana

“Tumefanya uamuzi huu kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni kutengeneza muunganiko mzuri kwa timu zote mbili, ya wanaume na wanawake lakini pia itatusaidia kuwajengea mabinti wetu kujiamini sana.

kwa upande mwingine Mratibu huyo amesema kuwa Pale Avic watapata nafasi ya kukutana na wachezaji wakubwa kama kina Mayele, Aziz KI, Feisal Salum na wengine hivyo kisaikolojia pia watakuwa wamepata maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo dhidi ya Simba Queens,” amesema Kibwana.

Kikosi cha Princess kitaanza mazoezi yake leo kuanzia saa 8:30 mchana kisha baadae wataipisha timu kubwa ya wanaume kufanya mazoezi.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI WA KAGERE KUSAJILIWA SINGIDA BIG STAR...PLUIJM NAYE NDANI YA NYUMBA....