Home Habari za michezo A-Z NAMNA BALEKE ALIVYOANZA SIMBA KWA MKWARA WA KUFA MTU….DODOMA WAFUNGWA GOLI...

A-Z NAMNA BALEKE ALIVYOANZA SIMBA KWA MKWARA WA KUFA MTU….DODOMA WAFUNGWA GOLI 12…

Habari za Simba

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Dodoma Jiji na Simba umemalizika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kwa wageni kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Bao hilo limefungwa na mshambuliaji mpya wa Simba Jean Baleke dakika ya 45 mara baada ya mabeki na kipa wa Dodoma Jiji, Daniel Mgore kushindwa kuokoa.

Baleke amejiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili akitokea TP Mazembe ya nchini Congo.

Zifuatazo ni dondoo muhimu za mchezo huu.

Tangu Dodoma Jiji ipande imecheza mechi sita dhidi ya Simba ambapo zote imepoteza ikifunga mabao mawili huku yenyewe ikifungwa mabao 12.

Takwimu zinaonesha katika mechi 11 ambazo Dodoma Jiji wamecheza wakiwa nyumbani wamepata ushindi mara nne na kupoteza saba huku wakifunga mabao nane na kufungwa mara 12

Mchezo wa mzunguko wa kwanza, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es salaam, goli la kujifunga la ,Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Habib Kyombo na Moses Phiri.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa nyota mpya wa Dodoma Jiji Raizin Hafidh ambaye ametokea Mbeya Kwanza.Katika mchezo huu,Raizin aliingia dakika ya 85 akichukua nafasi ya Muhsin Makame.

Huu ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara kwa Kocha Mkuu wa Simba Mbrazili, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ kukiongoza kikosi hicho na kupata ushindi tangu alipoteuliwa rasmi Januari 3, mwaka huu baada ya kuachana na mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Vipers.

Huu ni mchezo wa nne kwa kinda wa Dodoma Jiji, Fadhil Mwinyimkuu tangu apandishe timu ya wakubwa. Fadhil ambaye hucheza nafasi ya beki wa kulia ameanza katika michezo dhidi ya Tanzania Prisons,Mbeya City, Geita na Simba.

Katika mabao 14 yaliyofungwa na Dodoma Jiji, Colins Opare amefunga mabao manne akifuatiwa na Hassan Mwaterema mwenye mabao matatu.

Katika mabao 61 ya Simba, 10 yamefungwa na Mzambia Moses Phiri,John Bocco 9,Saido Ntibanzikiza 9 akiwa Simba na Geita)

Dodoma Jiji imefunga mabao 25 na kufungwa 15 huku ikipoteza michezo 12 Aishi Manula ameongeza idadi ya cleansheet akifikisha 11.

Katika mchezo huu, mwamuzi Tatu Malogo wa Tanga ametoa kadi za njano saba, Simba tatu na Dodoma Jiji nne.

SOMA NA HII  SIMBA YAGOMEA UBINGWA WAO KWENDA YANGA, HESABU ZAO HIZI HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here