Home Habari za michezo ALICHOKUWAFANYIWA NGASA NA YANGA…CHAMKUTA MAYELE…NI MWENDO WA SINDANO KILA MECHI…

ALICHOKUWAFANYIWA NGASA NA YANGA…CHAMKUTA MAYELE…NI MWENDO WA SINDANO KILA MECHI…

Habari za Yanga

Imebainika kuwa mshambuliaji kinara wa mabao Ligi Kuu Tanzania Bara anayekipiga kunako klabu ya Yanga, Fiston Kalala Mayele msimu uliopita wa 2021/2022 alicheza mechi tano akiwa mgonjwa akitaka kuisaidia timu yake ipate ushindi.

Hayo yamesemwa na mchambuzi wa Wasafi TV, George Job wakati akizungumzia usajili wa Kennedy Musonda raia wa aliyesajiliwa klabuni hapo ili kusaidiana na Mayele katika safu ya ushambuliaji.

“Yanga wamefanya usajili mzuri kulingana na mahitaji ya kikosi chao. Kuleta mshambuliaji mwingine ilikuwa ni lazima baada ya Kambole kuonesha uwezo mdogo na ilibidi Yanga wawe na mshambuliaji mwingine wa kumpa changamoto Mayele.

“Msimu uliopita Mayele kacheza zaidi ya mechi tano akiwa mgonjwa yote ni kwasababu yeye binafsi alitaka kuisaidia timu yake na timu ilihitaji huduma yake hivyo kumleta Musonda Kocha atakuwa na nafasi nzuri ya kumpumzisha baadhi ya mechi,” amesema Job.

Itakumbukwa kuwa , wakati Mrisho Ngasa akiichezea Yanga miaka hiyo, kulizuka taarifa za kuwa alikuwa akichomwa sindano za kutuliza maumivu ili aweze kucheza kwenye mechi mbalimbali za timu hiyo.

Kitendo hicho kinatajwa kuwa kilichangia kumkosesha dili la kucheza Uingereza kwenye klabu ya West ham United, ambapo timu ya madaktari kwenye klabu hiyo waligundua Ngasa alikuwa ni majeruhi wa muda mrefu.

SOMA NA HII  SIMBA QUEEN MGUU SAWA KAMA JESHINI NGAO YA JAMII