Home Habari za michezo AZIZ KI AONGOZA KWA KULIPWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI…MSHAHARA WAKE NI ‘GUNIA ZIMA’...

AZIZ KI AONGOZA KWA KULIPWA ZAIDI AFRIKA MASHARIKI…MSHAHARA WAKE NI ‘GUNIA ZIMA’ AISEE…

Habari za Yanga

Jarida la African Fact Zone limemuweka kiungo mshambxuiaji wa Yanga Stephane Aziz Ki Kama Idio mchezaji anayelipwa zaidi Tanzania.

Wameeleza kuwa Aziz Ki analipwa dola 10,700 kwa mwezi na kuwa ndio mchezaji anayelipwa zaidi katika soka la Tanzania na hata Afrika mashariki.

Dola 10,700 sawa na milioni 27 za Kitanzania huku wakienda mbali zaidi na kusema kuwa ada yaka ya usajili ilikuwa dola laki 2.15 yaani $215,000 ambazo ni sawa na milioni 502 za Kitanzania.

Ukiachana na staa huyo wa Yanga, wengine wanaolipwa mshahara mkubwa klabuni hapo kwa mujibu wa vyanzo vyetu ni pamoja na Fiston Mayele Mil 15, Yannic Bangala Mil 12, Khalid Aucho Mil 11, Jesus Moloko Mil 9.5 Gael Bigirimana Mil 8, Tuisila Kisinda Mil 7.

kwa upande wa mastaa wa kitanzania wanaocheza klabuni hapo anayeongoza kulipwa mshahara mkubwa analipwa mil 6 kwa mwezi, wakati kwa upande wa Simba anayeongoza kulipwa ni Clatous Chama anayelipwa Mil 16 huku anayemfuatia analipwa Milioni 12.

SOMA NA HII  NABI:- AZIZ KI HAKUCHEZA KWA MASLAHI YA YANGA...HAKUWA BORA KWANGU ...