Home Habari za michezo BAADA YA KUTAMBULISHWA…RONALDO AANZA KUWAPA MASHARTI WAARABU…

BAADA YA KUTAMBULISHWA…RONALDO AANZA KUWAPA MASHARTI WAARABU…

Cristiano Ronaldo

Rais wa Klabu ya Al Nassr, Musalli Al Muammar amesema kuwa staa wa timu hiyo Cristiano Ronaldo ameomba atendewe sawa na wachezaji wenzake ndani ya kikosi, asipendelewe.

“Wakati wa makubaliano, Ronaldo aliomba atendewe sawa na wachezaji wengine kikosini, kwenye upande wa zawadi za motisha na kanuni za timu.”- Musalli Al Muammar

Rais huyo wa Al Nassr ameongeza kuwa mshahara wake ni wa juu zaidi, huku akishindwa kutaja kiasi halisi cha fedha na kuongeza makubaliano yao yanamanufaa ya faida za kibiashara pia.

“Makubaliano na Ronaldo hayaishii kwenye mpira pekee, atasaidia pia kwenye Al Nassr Club Academy mpango ambao tumepanga pamoja na kuiwakilisha historia ya klabu.

SOMA NA HII  A-Z JINSI SAKHO ALIVYOFUTA AIBU SIMBA SC JANA...IHEFU 'WAENDELA KUBEBA WATU'...