Home Azam FC HAZIRA ZA SOPU ZAHAMIA KWA MANULA WA SIMBA…DENI LAKE LAZIDI KUKUA KILA...

HAZIRA ZA SOPU ZAHAMIA KWA MANULA WA SIMBA…DENI LAKE LAZIDI KUKUA KILA SIKU….

Habari za Michezo

Baada ya kumfunga Djigui Diarra mshambuliaji wa Azam FC, Abdallah Suleiman ‘Sopu’ amekiri kuwa anadeni na kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.

Iko; hivi Sopu amefanikiwa kumtungua kipa namba moja wa Yanga mabao matano kwenye timu mbili tofauti alianza kumfunga akiwa Coastal Union kwenye mchezo wa fainali Kombe la Shirikisho la Azam mechi iliyoisha kwa sare ya mabao 3-3.

Kwenye mchezo huo Sopu alifunga mabao yote matatu lakini hayakuwa na faida baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika na matokeo kuamuliwa na mikwaju ya penati Yanga wakitwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Mshambuliaji huyo alimfunga tena Diarra kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara msimu huu akiitumikia Azam FC kwa kutumbukiza mipira nyavuni mara mbili na kutoa asisti moja.

Sopu alisema mshambuliaji mkubwa anawafunga makipa wakubwa amefanya hivyo kwa Diarra anadeni kubwa na Manula ambaye ni kipa namba moja wa Simba na Taifa Stars.

Alisema ni furaha na farajia kubwa kwake kufunga kipa mkubwa ambaye ameonyesha uwezo ndani ya ligi huku akisisitiza kuwa si kumuweza bali ni namna anavyofanya maandalizi kumkabili mpinzani.

“Sio rahisi lakini inawezekana natambua ni kipa mzuri na amedhihirisha hilo kumfunga kwangu hakuondoi ubora wake mimi pia ninamipango yangu kuhakikisha nafanya kazi yangu kiwanjani ambayo ni kufunga,” alisema na kuongeza;

“Nitapambana kuhakikisha ninamfunga Manula ili niandike rekodi ya kuwafunga makipa wakubwa ambao naheshimu juhudi zao na ubora wao wawapo langoni kikubwa kila mmoja anatakiwa kutekeleza majukumu yake.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO....POLISI TZ WATAMBA 'KUIPELEKEA MOTO WA KUTOSHA' SIMBA...