Home Habari za michezo HUYU HAPA MTZ WA KWANZA KUMILIKI KLABU UINGEREZA…ALISEPA BONGO AKIWA ‘YANKI’ TU…

HUYU HAPA MTZ WA KWANZA KUMILIKI KLABU UINGEREZA…ALISEPA BONGO AKIWA ‘YANKI’ TU…

Mtanzania wa kwanza kumiliki klabu Uingereza

Klabu ya Oxford United iliyocheza na Arsenal na kupokea kichapo cha 3-0 kwenye kombe la FA imewahi kumilikiwa na Mfanyabiashara Firoz Kassam (68), mwenye asili ya India aliyezaliwa na kukulia Tanzania.

Akiwa na umri wa miaka 19 Kassam aliondoka Tanzania akaenda Uingereza kabla ya kuinunua klabu hiyo mnamo 1999 na kudumu nayo mpaka alipoiuza mnamo 2006.

Mwaka 2009 Kassam alitajwa kwenye Gazeti la The Times kama Mtu wa 309 kwa utajiri Uingereza akiwa na utajiri wa Pauni milioni 180.

Mnamo 2007, thamani yake ya jumla ilikadiriwa kuwa pauni milioni 240. Miaka 10 baadae thamani yake ilipanda mpaka pauni milioni 315 akitajwa kwenye orodha ya Matajiri ya Sunday Times ya 2017.

SOMA NA HII  WAKATI 'SKUDU' AKIRUDI ....TFF NAO WAANZA KUFANYA YAO KWA YANGA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here