Home Habari za michezo KAMA KAWA YANI…MORRISON KAIPIGA CHENGA YA MWILI YANGA…MASTAA WENGINE HAWA HAPA…

KAMA KAWA YANI…MORRISON KAIPIGA CHENGA YA MWILI YANGA…MASTAA WENGINE HAWA HAPA…

Habari za Yanga

Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa kihistoria Yanga Sc, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji wanne wa timu hiyo wataukosa mchezo wao dhidi ya IhefuĀ  leo.

Nyota hao wanne ni Azizi Ki raia wa BurkinaFaso, Bernard Morrison wa Ghana, Yanic Bangala wa DR Congo, Aboutwalib Mshery na Zawadi Mauya wa Tanzania kutokana na matatizo mbalimbali.

Inadaiwa kuwa Aziz Ki, Morrison na Bangala wamechelewa kujiunga na kambi huku Mauya akiwa majeruhi na Mshery amejitonesha jeraha.

Yanga wanashuka katika Dimba la Mkapa leo huku wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa na Ihefu kwenye mechi iliyotibua Unbeaten 49 za Wananchi.

Kwenye mchezo huo uliyopigwa Highland Estate mkoani Mbeya Yanga SC ilikufa kwa bao 2-1.

SOMA NA HII  KISA YANGA...SADIO KANOUTE ABAKI DAR WAKATI SIMBA WAKITUA MTWARA LEO...ISHU NZIMA IKO HIVI KUMBE...