Home Habari za michezo MIGOLI YA BOCCO NDANI YA SIMBA SC YAMTIA WAZIMU MAYELE…HATARI YAKE IKO...

MIGOLI YA BOCCO NDANI YA SIMBA SC YAMTIA WAZIMU MAYELE…HATARI YAKE IKO HAPA…

Habari za Simba SC

“Comeback” ya nahodha wa Simba SC, John Bocco imewaacha salama washambuliaji wawili tu, Fiston Mayele wa Yanga na Moses Phiri anayecheza naye timu moja, huku nao wakianza kupata presha.

Bocco hakuwa na mwanzo mzuri msimu huu, huku baadhi ya mashabiki wakimuandama kuona ni wakati wake wa kwenda kusomea ukocha ili uwanjani awachie damu changa, ingawa baadhi ya wachezaji wenzake walimkingia kifua.

Akiwa chini ya kocha Juma Mgunda, Bocco alirejea kwa kasi kuzitikisa nyavu, ambapo alianza na hat-trick timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mchezo uliopigwa Novemba 19, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Oktoba 2, 2022, kabla ya Bocco kutupia Reliants Lusajo wa Namungo alikuwa anamiliki mabao matano, Matheo Anthony (mabao manne), Fiston Mayele wa Yanga (matatu) na Moses Phiri (mabao matatu), Oktoba 5, Sixtus Sabilo wa Mbeya City alikuwa na mawili hao ni baadhi tu.

Kati ya hao waliomtangulia Bocco kucheka na nyavu, waliosalia salama ni Mayele ambaye ni kinara wa mabao 14 na Phiri mwenye 10 na sasa yupo nje ya uwanja kuuguza majeraha yake.

Bocco ana mabao tisa aliyofunga dhidi ya Ruvu(hat-trick), Polisi Tanzania akifunga moja kati ya mabao 3-1, Geita Gold alifunga moja katika ushindi wa mabao 5-0, KMC alifunga moja timu yake ikishinda 3-1 na Prisons hat -trick Simba SC ikishinda mabao 7-1.

Amewazidi waliomtangulia kufunga ambao ni Sabilo ambaye kwa sasa ana saba kazidiwa mawili, Idris Mbombo wa Azam FC ana saba kazidiwa mawili, Lusajo ana sita kazidiwa matatu, Matheo ana manne kazidiwa matano.

Ishu inayowafanya washambuliaji walioko mbele yake wapate presha ni kwa kuwa Bocco ana uwezo wa juu wa kufunga mabao zaidi ya moja kwenye mchezo mmoja tofauti na hao wengine ambao wamekuwa wakifunga moja moja au kwa nadra sana mawili kwenye mchezo mmoja.

Miongoni mwa wachezaji waliowahi kumkingia kifua Bocco kabla hajaanza kufunga ni Matheo aliwahi kusema “Bocco ni straika mzuri anastahili heshima yake, ana muendelezo wa kufunga binafsi nampa muda atafanya vizuri” wakati huo Matheo alikuwa na mabao manne.

Mwingine ni nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile alisema

“Bocco ni nembo ya vijana wengi wa kuiga mfano wa nidhamu yake, huwa naumia ninapoona mashabiki wakimshambulia, kitu kikubwa ni viongozi wake kumkingia kifua.”

Bocco ndiye mshambuliaji mahiri zaidi kwa sasa akiwa ameshafunga mabao 150 kuanzia ameanza kucheza Ligi Kuu Bara mwaka 2008.

SOMA NA HII  MANULA KUIKOSA TENA DABI YA KARIAKOO KISA HIKI HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here