Home Habari za michezo KIPA AFICHUA JINSI AZIZ KI ANAVYOBEBWA YANGA SC…AANIKA UZEMBE ULIPO…

KIPA AFICHUA JINSI AZIZ KI ANAVYOBEBWA YANGA SC…AANIKA UZEMBE ULIPO…

Azizi Ki akiwajibika Yanga SC

KIPA wa zamani wa Simba na Yanga SC, Said Mohammed ‘Nduda’ amesema licha ya frikiki za Stephan Aziz KI kuwa za kiwango lakini ni uzembe wa kipa kufungwa.

Aziz Ki, aliifungia Yanga SC bao pekee kwa mpira wa adhabu ambao kipa wa Mtibwa Sugar, Razack Shekimweri alishindwa kuudaka ukiwa ni muendelezo wa kufunga mabao ya aina hiyo.

Pia, alisababisha bao la faulo katika mchezo dhidi ya Azam dhidi ya kipa Ali Ahamada, na awali alifunga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba langoni akiwa Aishi Manula.

Nduda ambaye amewahi kuidakia Mtibwa Sugar, alisema ni uzembe uliopitiliza wa kipa kuruhusu mpira udunde mbele yake kwani ni lazima utampoteza maboya.

“Ukidunda hata ufanyaje huwezi kuudaka ninachokiona yale ni mabao rahisi sana na kipa ukifungwa lazima ujitafakari,” alisema Nduda ambaye ameichezea CDA ya Dodoma na Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Yanga SC.

Kipa huyo aliwashauri makipa kuwa na utaratibu wa kupanga mabeki warefu mwanzo wa ukuta ili kumfanya mpigaji ashindwe kuupitisha mpira.

“Mchezaji wa kwanza katika ukuta kulia ama kushoto ni lazima awe mrefu lakini kipa chungulia ukuta wako kabla mpira haujapigwa, makipa wengi hawafanyi hivyo ndio maana wanafungwa mabao ya kizembe,”alisema.

Hata hivyo, ameiangalia Ligi Kuu msimu huu na kudai ina ubora kutokana na timu nyingi kujipanga.

SOMA NA HII  MAKOCHA WAPISHANA KAULI ISHU YA BALEKE NA PHIRI KUACHWA PAMOJA SIMBA...ISHU HII HAPA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here