Home Habari za michezo KISA BARBARA KUJIONDOA SIMBA SC….ALLY KAMWE AFUNGUKA ALIVYOPATA SHIDA KUELEWEKA…

KISA BARBARA KUJIONDOA SIMBA SC….ALLY KAMWE AFUNGUKA ALIVYOPATA SHIDA KUELEWEKA…

Habari za Simba SC leo

Afisa Habari wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans Ally Shaban Kamwe, ameshindwa kuvumilia tukio lililomshawishi Baba yake mzazi kumtolea maneno mazito, baada ya Taarifa ya kujiuzulu kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Barbara Gonzalez.

Ally amezungumzia tukio hilo kuwa miongoni mwa matukio makubwa ambayo ameyashuhudia katika Siku 100 tangu alipoanza kazi Young Afrucans kama Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasilino.

Mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2022, Barabara alithibitisha kujiuzulu nafasi yake Simba SC, baada ya kuitumikia Klabu hiyo kwa zaidi ya miaka miwili, akichukua nafasi ya Senzo Mazingiza aliyetimkia Young Africans mwaka 2020.

Maamuzi ya kujuzulu kwa kiongozi huyo, yalipelekea Ally Kamwe kutoa kauli ya kuitania Simba SC huku akimsifia Afisa Mtendaji Mkuu wa Young Africans Andre Mtine, kitendo ambacho amesema kilimuibua Baba yake Mzazi na kumrushia maneno mazito.

“Wakati mtendaji mkuu wa Simba ametangaza kujiuzulu , nilifanya utani kwenye ukurasa wangu na kumsifia CEO wetu, huwezi kuamini nilitembelea ukurasa wa Mzee wangu aliongea maneno sikuamini,”

“Huyu ni Baba yangu mzazi lakini sababu nilimtania Mtendaji wake akanitolea maneno ambayo tukikaa nyumbani hawezi kunitolea, Mzee amenitazama kama Afisa habari wa Yanga sio mwanaye.” amesema Ali Kamwe

Mashabiki, Wanachama na Viongozi wa Klabu za Simba SC na Young Africans wamekua na kasumba ya kuendeleza itikadi za Utani kwa matukio mazuri na mabaya yanayozikumba Klabu hizo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kwa nyakati tofauti.

SOMA NA HII  KUELEKEA NUSU FAINAL...BALEKE NA MAYELE WATABIRIWA MAKUBWA CAF...