Home Habari za michezo KISA MICHUANO YA CAF….MBRAZILI ATIMKA SIMBA…ARUDI KWAO BRAZIL USIKU USIKU..

KISA MICHUANO YA CAF….MBRAZILI ATIMKA SIMBA…ARUDI KWAO BRAZIL USIKU USIKU..

Habari za Simba

Kikosi cha Simba SC kinarejea kwenye mazoezi leo Jumanne, Januari 24, 2023 lakini Kocha Mbrazili, Roberto Oliveira Robertinho jana usiku aliondoka nchini kwenda kwao Brazil.

Taarifa za ndani zinaeleza kuwa sababu iliyomfanya Robertinho kuondoka nchini ni hati yake ya kusafiria kumalizika muda wake na hakuna hata karatasi moja iliyo wazi na hivi karibuni atatakiwa kuanza kusafiri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Hapa nchini hakuna Ubalozi wa Brazil kwa hiyo Robertinho atakwenda kwao kufuatilia Pasipoti ili kupata mpya na ataanza kuitumia kwenye safari ya kwanza kwenda Guinea katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya.

Hata hivyo, taarifa ya Simba SC imesema Roberto Oliveira ameondoka kwenda nchini kwao Brazil kwa shughuli binafsi za kifamilia na anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA:SIMBA HAIKUPASWA KUMSAJILI CHIKWENDE