Home Habari za michezo KISA ‘MVUA YA MAGOLI’….MBEYA CITY WAPAZA SAUTI KUHUSU TABIA ZA SIMBA KWA...

KISA ‘MVUA YA MAGOLI’….MBEYA CITY WAPAZA SAUTI KUHUSU TABIA ZA SIMBA KWA MAGOLIKIPA…

Habari za Simba

Baada ya kukumbana na kipigo kizito katika mchezo uliopita, Kocha wa makipa wa Mbeya City, Ally Mustapha ‘Bartez’ amesema hawatarajii tena kuaibishwa Dar es Salaam akisema eneo la golini limeimarika hivyo Simba wasitarajie mteremko.

Mbeya City ilifunga mwaka kwa aibu ilipochapika kwa idadi kubwa ya mabao 6-1 dhidi ya Azam na keshokutwa Jumatano itawavaa Wekundu, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba inawakaribisha wapinzani hao ikikumbuka ushindi mnono ilioupata kwenye mchezo uliopita ilipoifunga Prisons mabao 7-1, huku ikitoa sare ya 1-1 dhidi ya City walipokutana mzunguko wa kwanza Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mbeya City wapo nafasi ya 10 kwa pointi 21, huku Simba ikiwa nafasi ya pili kwa alama 44 baada ya pande zote kushuka uwanjani mara 19 na kufanya mechi hiyo kuwa na upinzani mkali.

Bartez alisema upungufu ulioonekana kwenye mechi iliyopita wamekuwa na muda mzuri wa maandalizi na kurekebisha kasoro zote, hivyo hawaamini kurudia makosa.

“Kwa upande wa golini sina wasiwasi kabisa, tumefanyia kazi makosa tangu tumalize mechi na Azam, hivyo Simba wasitarajie mteremko, tunaenda kufanya kweli na kuwapa raha mashabiki,” alisema kocha huyo.

Straika na kinara wa mabao kikosini humo, Sixtus Sabilo alisema baada ya kuhaha kwa muda mrefu na matokeo yasiyoridhisha sasa kazi inaanza upya dhidi ya Simba akitamba kupata pointi tatu.

“Ni muda mrefu tumepata ushindi, naamini kwa muda wa mapumziko tumerekebisha mambo mengi na sisi wachezaji kazi yetu ni kuwapa raha mashabiki na tunaenda kuanza na Simba,” alitamba Sabilo mwenye mabao saba.

SOMA NA HII  HUKUMU YA JONAS MKUDE YAAHIRISHWA