Home Habari za michezo KUHUSU BALEKE KUSAJILIWA KWA MKOPO…BOSI SIMBA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA MKATABA ULIVYO…

KUHUSU BALEKE KUSAJILIWA KWA MKOPO…BOSI SIMBA AVUNJA UKIMYA…AFUNGUKA MKATABA ULIVYO…

Habari za Simba

Baada ya kuenea kwa taarifa kuhusu usajili wa mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke kwamba ametua hapo kwa mkopo akitokea TP Mazembe, uongozi  umeibuka na kutoa ufafanuzi.

Baleke raia wa DR Congo, amejiunga na wekundu wa msimbazi katika usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu.

Meneja wa Habari na mawasiliano wa Mabingwa hao wa zamani wa Ligi Kuu, Ahmed Ally, alifunguka kuwa: “Tetesi au maneno yanayoendelea kuhusu mkataba wetu na Jean Baleke kuwa tumemchukua kwa mkopo sio za kweli.

“Baleke tumemsajili katika dirisha dogo la usajili kwa kandarasi ya miaka miwili kutoka TP Mazembe, kwa hiyo tutakuwa na Belake mpaka 2025.

“Eneo la straika lilikuwa na nafasi moja ya wazi, kwa hiyo tusingeweza kujaza nafasi hiyo kwa kumchukua mchezaji kwa mkopo, Simba hatuna tamaduni hiyo na malengo yetu hayaendani na taratibu hizo.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUMALIZANA NA NTIBAZONKIZA....SINGIDA BIG STARS YASHUSHA KIFAA HIKI KINGINE...MAKAMBO NAYE NDANI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here