Home Habari za michezo KWA TAKWIMU HIZI….YANGA WALIIINGIA CHA KIKE KWA MORRISON…

KWA TAKWIMU HIZI….YANGA WALIIINGIA CHA KIKE KWA MORRISON…

Habari za Yanga

Klabu ya Yanga walimuacha mchezaji wao Saido Ntibazonkiza kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu na wakamsajili Bernard Morrison alieachwa na Simba kwa sababu ya utovu wa nidhamu.

Simba nao wakaachana na Bernard Morrison huku ikielezwa utovu wa nidhamu ni sehemu ya sababu zilizotajwa kuwatenganisha na dirisha hili wamemuongeza Saido Ntibazonkiza alieachwa na Yanga kwa sababu ya utovu wa nidhamu.

Saido alipoondoka Yanga alikwenda Geita Gold alikofunga jumla ya mabao manne na assist 6, na tangu amejiunga na Simba amecheza mchezo mmoja aliofunga mabao matatu na assist moja.

Bernard Morrison akiwa Yanga amecheza jumla ya michezo 10 Kati ya 19 huku akifunga mabao mawili na assist mbili.

Mpaka sasa takwimu zinambeba Saido Ntibazonkiza dhidi ya Bernard Morrison huku takwimu za Morrison tangu ajiunge na Yanga (kahusika katika mabao 4) Ntibazonkiza amezitengeneza katika mchezo mmoja tu akiwa na uzi wa Simba.

Lakini pia, Morrison amekuwa na matukio mengi nje ya uwanja huku akiripotiwa kuwa na utovu wa nidhamu na kuchelewa kuwasili kambini nk, wakati huo kwa upande wa Ntibazonkiza hajaripotiwa kuwa na utovu wa nidhamu tangu aondoke Yanga.

SOMA NA HII  NABI AMPA WOSIA HUU AZIZ KI...AMCHANA MAKAVU LIVE...AMEZUNGUMZA HAYA