Home Habari za michezo RASMI….MSUVA HUYOOO MBEYA CITY….MAMBO YOTE YAKO HIVI πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯….

RASMI….MSUVA HUYOOO MBEYA CITY….MAMBO YOTE YAKO HIVI πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯πŸ”₯….

Msuva na mdogo wake

Klabu ya Mbeya City iko kwenye hatua za mwisho za kunasa saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Singida Big Stars, James Msuva kwa mkataba wa miezi sita utaomuweka hadi mwishoni wa msimu.

Taarifa ambazo gazeti laΒ  Mwanaspoti imepenyezewa ni kwamba dili hilo litakamilika muda wowote kwani wawakilishi wa klabu zote mbili wamekutana huku ikielezwa mchezaji mwenyewe amekubali.

“Tulifanya kikao na viongozi wa Singida na tunashukuru mazungumzo yameenda vizuri hivyo tunachosubiri ni mambo machache ya kukubaliana hususani kwenye malipo,” kilisema chanzo hicho.

Akizungumzia usajili huo kocha msaidizi wa Mbeya City, Anthony Mwamlima alisema wamekuwa na vikao mbalimbali juu ya kuboresha kikosi chao hivyo muda utakapofika wataweka wazi.

“Kuna wachezaji ambao tumewaomba kwa mkopo hadi mwisho wa msimu lakini siwezi kuwataja hapa, tunasubiria tutakapokamilisha tutawaweka wazi hivyo endelea tu kusubiri,” alisema.

Mkurugenzi wa ufundi wa Singida, Ramadhan Nswanzirimo alisema lengo lao kubwa ni kuwatoa wachezaji kwa mkopo ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza mara kwa mara.

James ambaye ni mdogo wake, Simon Msuva amewahi kuzichezea timu za vijana za Simba, JKT Ruvu na Yanga kabla ya kutua Mbao iliyokuwa inanolewa na Etienne Ndayiragije, KMC kisha Ruvu Shooting.

SOMA NA HII  ACHANA NA STORI ZA VIJIWENI...HUU HAPA UKWELI WA KWANINI KAMBOLE HATACHEZA MECHI YA LEO DHIDI YA SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here