Home Habari za michezo SABILO WA MBEYA CITY KUIBUKIA SIMBA SC….ATULIZA PRESHA….JAMBO LITAKUWA HIVI…

SABILO WA MBEYA CITY KUIBUKIA SIMBA SC….ATULIZA PRESHA….JAMBO LITAKUWA HIVI…

Habari za Simba

Straika wa Mbeya City, Sixtus Sabilo amesema kupungua kwa kasi yake uwanjani kumesababishwa na matokeo ya jumla ya timu baada ya kupitia kipindi kigumu, akiahidi kurejesha katika ubora wake kuanzia mechi ijayo dhidi ya Simba.

Sabilo alikuwa na mwanzo mzuri akitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania tuzo ya kiatu cha mfungaji bora msimu huu, lakini kwa sasa ameonekana kukata pumzi akiachwa mbali na wapinzani akiwamo kinara wa mabao Fiston Mayele (14) wa Yanga.

Sabilo alikiri kuwa kiwango chake kwa sasa kimepungua na yote ni kutokana na matokeo ya timu kutokuwa mazuri baada ya kipindi kigumu walichopitia ndani na nje ya uwanja.

Alisema mara zote mpira huwa na matokeo ya kusikitisha na kufurahisha, hivyo anaamini kuanzia mchezo ujao dhidi ya Simba Januari 17 anaweza kuanza tena upya kukimbiza uwanjani.

“Japokuwa malengo yangu siyo kuwania ufungaji bora lakini nahitaji kuona kasi inarejea kama ilivyokuwa mwanzo, timu kama haifanyi vizuri ni nadra sana mchezaji kung’ara, hivyo najipanga upya,” alisema Sabilo.

Nyota huyo aliongeza kuwa mapumziko mafupi waliyonayo kwa sasa yatasaidia kufanya marekebisho ya kikosi chao ili kuisaidia Mbeya City kuondokana na mzimu wa kupata matokeo yasiyoridhisha.

Aliwaomba mashabiki na wadau wa timu hiyo kutokata tamaa akibainisha kuwa mechi zilizobaki watapambana kadri ya uwezo wao kuhakikisha wanarejesha furaha na tabasamu.

“Lazima tutumie kipindi hiki kusahihisha makosa yetu ndani ya uwanja kuweza kuwapa raha mashabiki wetu, bado malengo ni yale kumaliza ndani ya nafasi nne za juu hivyo tunaomba wasikate tamaa,” alisema straika huyo.

SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA