Home Habari za michezo HUKO SIMBA SC JAMBO SI JAMBO…MGUNDA KAIBUKA NA RIPOTI HII KUHUSU NTIBAZONKIZA…

HUKO SIMBA SC JAMBO SI JAMBO…MGUNDA KAIBUKA NA RIPOTI HII KUHUSU NTIBAZONKIZA…

Habari za Simba

KIWANGO bora ilichokionyesha Simba SC wiki iliyopita kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ikishinda 7-1 dhidi ya Tanzania Prisons, kimemfanya kocha mkuu wa chama hilo, Juma Mgunda kuweka wazi kuwa amepata alichokuwa anakitafuta na sasa ni mwendo wa kutembeza dozi tu, huku akisema Saido Ntibazonkiza ana faida kubwa sana kwenye timu yake kwa sasa.

Katika mchezo huo, Simba SC ilionekana kumiliki mpira kwa asilimia nyingi na kucheza kwa maelewano makubwa hususani kuanzia eneo la kiungo na ushambuliaji jambo lililowafanya mashabiki wa timu hiyo kutamba lakini Mgunda amefunguka ubora huo amekuwa akiutengeneza mazoezini.

Tambo hizo zilichagizwa na ubora aliouonyesha nyota mpya wa Wanamsimbazi hao, Saido aliyefunga ‘hat trick’ na kutoa asisti moja kwenye mechi hiyo ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kikosini hapo tangu asajiliwe kwenye dirisha dogo hili akitokea Geita Gold na kubwa zaidi ikiwa ni namna alivyoonyesha kuwa na maelewano makubwa ya kiuchezaji na mastaa wengine wa Simba SC kama Clatous Chama, Pape Sakho, Mzamiru Yassini na John Bocco.

Mgunda alisema amefurahishwa na ushindi huo mkubwa zaidi kwenye Ligi Kuu hadi sasa msimu huu na anawapongeza wachezaji wa Simba SC kwa kufanyia kazi kile alichowaelekeza mazoezini na kupata ushindi.

“Ni matokeo mazuri, nimefurahi na nimeona ni namna gani tunaweza kucheza mechi nyingine na kupata matokeo chanya kama haya.

“Hivi ni miongoni mwa vitu tulivyokuwa tunavitaka na tunavifanyia mazoezi, tunataka kuiona timu ikicheza vizuri, ikishinda na kuburudisha na imekuwa hivyo nimefurahi,” alisema Mgunda.

SAIDO ANOGESHA MIFUMO

Katika nafasi nyingine, Mgunda alikiri, Simba SC ilikuwa inahitaji mchezaji wa kiwango kama cha Saido na ujio wa Mrundi huyo ndani ya kikosi chake utaongeza ubora kwenye uchezaji pia utampa machaguo tofauti ya mifumo.

“Saido ana uzoefu wa kutosha na ana uwezo mkubwa sana, kwa timu niliyonayo tulihitaji mtu kama huyo na amekuja kuleta kitu cha nyongeza kikosini kama mlivyoona,” alisema Mgunda na kuongeza;

“Uwepo wake utatupa nafasi hata sisi benchi la ufundi kuwa na aina nyingi za mifumo kwani anaweza kucheza eneo zaidi ya moja uwanjani na kwa bahati nzuri amezoeana na wenzake kwa muda mfupi.”

SOMA NA HII  MABOSI SIMBA WAANZA KUYAPANGIA BAJETI MABILIONI YA CAF SUPER LEAGUE...BAJANA ATAJWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here