Home Habari za michezo WAKATI SIMBA WAKIJIDAI NA DUBAI…YANGA WAMETULIA ZAO TULIII…ILA MZIKI WAKE SIO POA...

WAKATI SIMBA WAKIJIDAI NA DUBAI…YANGA WAMETULIA ZAO TULIII…ILA MZIKI WAKE SIO POA AISEE..

Tetesi za Usajili Yanga

Yanga inaendelea na usajili wa dirisha dogo na mpaka sasa kuna staa mmoja wameshamtambulisha na mwingine ni suala la muda tu, lakini watu hao wawili wanazidi kuleta mshtuko mkubwa kuitia presha ya upangaji wa kikosi chao kwa sasa.

Yanga hadi sasa imeshamtambulisha kiungo Mudathir Yahya kuwa staa wao wa kwanza kumsajili karika dirisha dogo na alianza kukiwasha kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023, huku mshambuliaji Mzambia Kennedy Musonda akibakiza hatua chache naye kuja kuvaa uzi wa wananchi.

Ujio wa watu hao wawili tu unaleta picha mbili za vikosi viwili vilivyo bora kushindana katika mechi yoyote ya ligi huku mastaa wengine 7 wakiwa nje ya vikosi hivyo.

UKUTA BALAA

Katika kikosi cha kwanza  ukuta wa Yanga unaweza kuwa ule ule ambao unasumbua ukiwa na kipa Djigui Diarra, beki wa kulia akiwa Kibwana Shomari, kushoto akienda Lomalisa Mutambala huku mabeki wa kati wakiwa Dickson Job na Yannick Bangala.

KUNGO USISEME

Safu ya kiungo inaweza kuwa na mabadiliko kidogo akiingia Mudathir ambaye atacheza sambamba na Khalid Aucho, Jesus Moloko akianzia winga ya kulia huku Stephan Aziz KI akiwa nyuma kidogo ya mshambuliaji wa mwisho.

MBELE SASA

Safu ya ushambuliaji kinara wa mabao katika ligi na hata hapo Yanga Fiston Mayele atakuwa na uhakika huku pembeni kidogo akicheza ingizo jipya Musonda ambaye kwa kasi yake na nguvu atakuwa na ubora wa kucheza nusu ya eneo (Half space) hilo kuleta uwiano.

KIKOSI CHA PILI

Kikosi cha pili nacho kitakuwa na moto wake ambapo golini ataanza kipa mzawa Aboutwalib Mshery, beki wake wa kulia akiwa Djuma Shaban,nahodha mkuu Bakari mwamnyeto akicheza sambamba na Ibrahim Bacca kama mabeki wa kati huku beki wa kushoto akicheza David Bryson.

SURE BOY, KISINDA

Safu ya kiungo kuna watu wanne wakianza na Zawadi Mauya,Salum Aboubakar ‘Sure boy’, winga wa kulia akiwa Tuisila Kisinda, huku Farid Mussa akicheza nyuma kidogo ya mshambuliaji wa mwisho.

MZIZE NA BM33

Safu ya ushambuliaji itakuwa chini ya Clement Mzize akicheza sambamba na Bernard Morrison ambaye anajua kulainisha mashambulizi kwa ufundi wake.

SABA BENCHI

Mbali na kikosi hicho kutakuwa na mastaa wengine 7 wako nje wakisubiri nafasi katika vikosi hivyo ambani ni kipa Erick Johola,beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’, viungo wakiwa Gael Bigirimana,Dickson Ambundo, Feisal Salum ambaye yuko katika mgogoro na klabu yake,Denis Nkane na mshambuliaji Crispin Ngushi.

MSIKIE NABI

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi alisema kwasasa hataki kuzungumzia juu ya usajili unaondelea kufanyika mpaka utakapokamilika lakini amefurahishwa na ujio wa Mudathir akisema utaongeza ushindani zaidi eneo la kiungo.

“Bado hatujamaliza kazi katika kuboresha timu lakini nimefurahi kupatikana kwa Mudathir, huyu ni kiungo ambaye namjua ubora wake naamini naweza kuwa na mengio ya kueleza wakati ukifika hasa baada ya usajili kukamilika, kitu muhimu tunatka kuongeza watu bora ambao watakuja kuongeza ushindani wa nafasi,” alisema Nabi.

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Yanga na Taifa Stars aliyetamba pia na Tukuyu Stars, Sekilojo Chambua alisema amekoshwa na ujio wa Mudathir katika kikso chao kwa kuwa uwezo wake unajulikana lakini pia anaona zitakuwa habari njema kama Yanga itamalizana na Musonda.

“Sina uhakika sana juu ya taarifa za Musonda lakini niseme kama atasajiliwa mshambuliaji hizo zitakuwa taarifa njema kwa kuwa tuna uhitaji wa mshambuliaji mwingine ambaye atakuja kuongeza nguvu katika mashindano ambayo tunacheza,”alisema Chambua.

“Tumeona usajili wa Mudathir sote tunamjua kwamba ni kiungo mzuri ana uwezo mkubwa wa kukaba na hata kushambulia, ujio wake ndani ya Yanga utaongeza kitu kikosini,” alisisitiza gwiji huyo.

KIKOSI I

Diarra Kibwana Lomalisa Job Bangala Aucho Mudathir Moloko Mayele Aziz KI Musonda

KIKOSI II

Mshery Djuma Bryson Mwamnyeto Bacca Mauya Sure boy Kisinda Mzize Morrison Farid

AKIBA

Gael Johola Ambundo Nkane Ninja Ngushi Feisal

SOMA NA HII  SAA MOJA KABLA YA KUKIPIGA NA WAARABU...MATOKEO YAIBEBA YANGA..NABI AINGIA KININJA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here