Home Habari za michezo AL AHLY YA MISRI NA AS VITA WALIA PAMOJA NA SIMBA KUFUNGWA...

AL AHLY YA MISRI NA AS VITA WALIA PAMOJA NA SIMBA KUFUNGWA LIGI YA MABINGWA AFRIKA…

Simba vs Raja

WAKATI Raja Casablanca ikiichapa Simba mabao 3-0 pale uwanja wa taifa jana na Yanga ikipata ushindi wa mabao 3-1 jana mbele ya TP Mazembe, mambo yanaonekana kuwa magumu kwa vigogo wa Afrika kwa msimu huu kwani hata bingwa mtetezi hana hata alama moja.

Wydad Casablanca ambayo ilichukua ubingwa msimu uliopita hadi sasa inashika nafasi ya mwisho kwenye kundi A, ikiwa imecheza mechi moja na dhidi ya JS Kabylie na kupoteza kwa mabao 1-0.

Al Ahly ambayo msimu uliopita ilicheza fainali dhidi ya Wydad nayo hadi sasa haina alama hata moja ikiwa inashika nafasi ya tatu kwenye kundi B, baada ya kucheza mechi moja dhidi ya Al Hilal na kupoteza.

Zamalek ambao ni wapinzani wa karibu na Al Ahly kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye kundi D ina alama moja tu ikiwa imecheza mechi mbili.

Al Ahly na Wydad zimecheza mechi moja moja kwa kuwa walikuwa kwenye majukumu ya michuano ya Klabu Bingwa Dunia iliyokuwa inafanyika Morocco.

Kigogo mwingine wa Afrika ambaye hadi sasa hajaambulia alama hata moja ni AS Vita ambayo iliwahi kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2018. Vita imecheza mechi mbili za hatua ya makundi na zote imepoteza.

SOMA NA HII  LIGI YA MABINGWA AFRIKA: SIMBA 1-0 AL AHLY