Home Habari za michezo ALIYESHINDWA NA MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA…AFICHUA YALIYOTOKEA KWENYE KARATASI ZA MATOKEO…

ALIYESHINDWA NA MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA…AFICHUA YALIYOTOKEA KWENYE KARATASI ZA MATOKEO…

Mkutano Mkuu Simba Leo

Wakili Moses Kaluwa, aliyekuwa anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Simba kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi Jumapili, ameweka wazi kuwa, hajaridhishwa na matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Murtaza Mangungu.

Kaluwa alisema, ameshindwa kusaini karatasi ya kukubali matokeo hayo ya uchaguzi kwa kuwa hajakubaliana nayo, ingawa uamuzi wake huo hauwezi kubadilisha lolote.

Mangungu ameshinda uchaguzi huo na kutetea nafasi ya mwenyekiti kwa kupata kura 1,311, wakati Kaluwa akivuna kura 1,045 kwenye matokeo ya uchaguzi huo ambayo yalitolewa alfajiri ya jana Jumatatu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Simba, Boniface Lihamwike.

“Sijaridhishwa na matokeo na sijasaini karatasi ya matokeo kuonesha kukubali kwa kuwa msimamo wangu upo wazi. Ila ombi langu kwenu ni kuwa Klabu ni kubwa kuliko uchaguzi.

“Simba ni kubwa kuliko sisi, wote tunajukumu kubwa la kuijenga Simba, tunaipenda Simba, hatupendi watu. Hata kama sijasaini ila nitashirikiana na wenzangu.

“Zile sera na hoja zangu, walizisikia wanaweza kuzifanyia kazi na kuziboresha kama zitakuwa na mapungufu,” alisema.

SOMA NA HII  SIMBA WAPEWA SIRI ZA 'UCHAWI' WA FEI TOTO...WAAMBIWA JINSI UNAVYOTUMIKA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here