Home Habari za michezo BAADA YA KUONA WENZAKE WAKIZIDI ‘KUSHINE’ …PHIRI ‘AFOSI’ JAMBO SIMBA…

BAADA YA KUONA WENZAKE WAKIZIDI ‘KUSHINE’ …PHIRI ‘AFOSI’ JAMBO SIMBA…

Habari za Simba

Mshambuliaji kinara wa Simba, Moses Phiri ameahidi kurejesha makali yake na kuendelea kufunga mabao baada ya kupona majeraha.

Phiri amesema ushindani wa namba kwenye kikosi cha Simba umekuwa mkubwa baada ya kuongezwa wachezaji wapya lakini atapambana kurudisha nafasi yake.

“Nina furaha nimerudi, sio kitu kizuri kwa mchezaji kukosa mechi nyingi kutokana na majeruhi lakini nimejipanga kuhakikisha narudi kwa nguvu kama nilivyoanza msimu.”

“Kwa sasa niko fiti baada ya mchezo dhidi ya Singida nitakuwa tayari kucheza, nimejipanga kuhakikisha naendeleza ubora wangu.”

Akizungumzia kuhusu ujio wa mshambuliaji, Jean Baleke, Phiri amesema “Ni mchezaji mzuri, ana kasi pia anajua kufunga naamini ataisaidia timu.”

SOMA NA HII  MASHABIKI WACHOMA MOTO UWANJA...LIGI YA MABINGWA AFRIKA...ISHU NZIMA HII HAPA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here