Home Habari za michezo BAADA YA KUONA YANGA WAMESIMAMIA UKUCHA…MBRAZILI SIMBA AIBUKA NA RAMANI MPYA…

BAADA YA KUONA YANGA WAMESIMAMIA UKUCHA…MBRAZILI SIMBA AIBUKA NA RAMANI MPYA…

Habari za Simba SC

Kocha Mkuu Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema, ili kufanikisha ndoto za kutwaa ubingwa msimu huu 2022/23 kwa klabu hiyo, ni lazima kikosi chake kishinde michezo yote iliyosalia.

Simba SC kesho itashuka katika Dimba na Benjamin Mkapa kupapatuana na Singida Big Stars, katika mchezo wa Mzunguuko wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha Robertinho ametoa kauli hiyo baada ya kurejea nchini na kuanza kazi mara moja, jana Jumatano (Februari Mosi) majira ya jioni, Uwanja wa Mo Simba Arena.

Kocha huyo kutoka nchini Brazil amesema: “Tunahitaji kushinda ubingwa wa Ligi, ili kukamilisha hilo lazima tushinde michezo yote iliyobaki huku tukiangalia wapinzani wetu aina ya matokeo yao, na uzuri wake tuna mchezo nao, tukishinda tunazidi kupunguza alama walizonazo.”

Simba SC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikizidiwa alama sita dhidi ya vinara Young Africans yenye alama 56.

SOMA NA HII  WAKATI WENGINE WAKIPEWA 'THANK YOU'....YANGA NA SURE BOY MAMBO NI HIVI 🔥🔥🔥...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here