Home Habari za michezo BAADA YA KUSIKIA TETESI ZA KUTAKIWA NA YANGA…BRUNO KAACHEEKAA…KISHA AKASEMA HILI…

BAADA YA KUSIKIA TETESI ZA KUTAKIWA NA YANGA…BRUNO KAACHEEKAA…KISHA AKASEMA HILI…

Tetesi za Usajili Yanga SC

Kiungo kutoka nchini Brazil na Klabu ya Singida Big Stars Bruno Barroso amekanusha uvumi unaoendelea kuhusu mpango wa kusajiliwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC.

Bruno amekua akitajwa sana kuwa kwenye mpango wa kuhamia Yanga mwishoni mwa msimu huu, kufautia kuonesha kiwango bora tangu alipotua Singida Big Stars.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Simba SC jana Ijumaa (Februari 03), Kiungo huyo amesema hafahamu lolote kuhusu Yanga, lakini amekua wakisikia taarifa za kuhusishwa na klabu hiyo ya Dar es salaam.

Amesema anachotambua kwa sasa yeye ni mchezaji wa Singida Big Stars na yupo klabuni hapo kwa misingi na taratibu za mkataba, kwa hiyo hawezi kusema lolote kuhusu mpango huo wa usajili wa kwenda kwingine mwishoni mwa msimu huu.

“Nimejitolewa kuja Tanzania kwa ajili ya kuitumikia Singida Big Stars, ndio maana ninacheza kwa moyo wangu wote na kuisaidia timu kama mnavyoona, sijui lolote kuhusu mpango wa kwenda klabu nyingine.”

“Nimekua nasikia taarifa za mimi kutakiwa Young Africans, lakini ukweli ni kwamba sifahamu lolote kuhusu hilo na ninasisitiza nipo hapa Singida Big Stars kwa mapenzi na nitaendelea kupambana kwa ajili ya klabu hii.” amesema Bruno

SOMA NA HII  BABA LEVO: KAMA YANGA IKIFUNGWA NA SIMBA DIAMOND ANIFUKUZE KAZI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here