Home Habari za michezo BAADA YA OKWA NA AKPAN KUTUA IHEFU…KATWILA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA JIPYA HILI…

BAADA YA OKWA NA AKPAN KUTUA IHEFU…KATWILA ASHINDWA KUJIZUIA…AIBUKA NA JIPYA HILI…

Habari za Simba

Viungo Victor Akpan na Nelson Okwa bado hawajapewa muda mwingi Ihefu, lakini inalezwa ujio wao kwenye timu hiyo umeongeza mzuka kwani kila mchezaji kwa sasa anajituma mara mbili zaidi ili acheze kikosi cha kwanza tofauti na mwanzoni.

Kocha Mkuu wa Ihefu, Zubery Katwila alisema siri kubwa ya wao kufanya vizuri katika michezo ya hivi karibuni ni uwepo wa nyota hao.

“Timu inapokuwa na wachezaji bora kwenye kila maeneo inaongeza ushindani sana na hata timu kiujumla inafanya vizuri kwa sababu kuna wengine wanaona hawana upinzaji katika nafasi zao hivyo wanapokuwa wengi wenye ubora lazima wahofie nafasi zao.”

Katwila aliongeza ni kweli Okwa na Akpan hawajapata dakika nyingi za kucheza kwani anawaingiza taratibu taratibu kwenye kikosi chake ili kutengeneza muunganiko mzuri na bora ambao utaleta tija katika michezo yao minane migumu iliyosalia.

“Mchezaji anachaguliwa kuanza kikosi cha kwanza kutokana na aina ya mchezo na mpinzani tunayecheza naye, ni kweli mara nyingi wanatokea benchi lakini kama nilivyosema mwanzoni uwepo wao tu umeleta mapinduzi makubwa kwenye timu,” alisema.

Ihefu imekuwa na matokeo mazuri kwani katika michezo yake mitano iliyopita imeshinda minne na kupoteza mmoja ikishika nafasi ya saba na pointi 26 baada ya kucheza michezo 22 ambapo kati ya hiyo imeshinda minane, sare miwili na kupoteza 12.

SOMA NA HII  VIDEO: SHABIKI ALIYEJICHORA NEMBO YA SIMBA ATAJA SABABU YA KUIPENDA TIMU HIYO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here