Home Azam FC BEKI AZAM FC ALIA NA KIBU DENIS….AMTUPIA LAWAMA KWA KUMCHANGANYA….

BEKI AZAM FC ALIA NA KIBU DENIS….AMTUPIA LAWAMA KWA KUMCHANGANYA….

Habari za Simba

Baada ya kujifunga bao la dakika za mwishoni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, beki wa Azam FC, Abdallah Heri ‘Sebo’ ameeleza namna ilivyokuwa hadi kujifunga.

Sebo alijifunga katika dakika ya 90 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya Wanalambalamba kuanza kuongoza kwa bao lililofungwa katika sekunde ya 13 na Prince Dube.

Akizungumza , Sebo alisema kona iliyochochongwa na mshambuliaji wa Simba, Kibu Denis ilimpotezea muelekeo na kujikuta anakwamisha mpira nyavuni mwao kwa kichwa badala ya kuokoa.

“Nimejisikia vibaya kama mchezaji lakini ni lazima nikubali kwasababu makosa yameshatokea na mchezo mwingine yeyote anaweza akakosea.

“Naomba radhi kwa benchi la ufundi, wachezaji wenzangu na mashabiki wa Azam FC kwa kile kilichotokea kwasababu sikufanya makusudi, ni ajali kazini nikiwa kwenye harakati za kuokoa nikajikuta najifunga.”

Akizungumzia mchezo kwa ujumla Sebo alisema ulikuwa ni mgumu kwa kila pande kutokana na timu zote kuhitaji pointi tatu huku akikiri kuwa wao walipata nafasi nyingi lakini walikosa umakini kwenye kuzitumia na kujikuta wanaambulia pointi moja.

“Malengo yetu hayajatimia, msimu huu tulitaka kukusanya pointi zote sita kutoka kwa Simba lakini ukosefu wa umakini umetufanya tuambulie pointi nne, sio haba tutajipanga zaidi kwenye michezo iliyobaki kuhakikisha tunakusanya pointi zote.”

SOMA NA HII  SIMBA KUREJEA BONGO LEO, WAPANIA KUPINDUA MEZA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here