Home Azam FC DUBE AANIKA SIRI ZA NDAANI KABISA ZA KUMTUNGUA MANULA KILA WAKICHEZA NA...

DUBE AANIKA SIRI ZA NDAANI KABISA ZA KUMTUNGUA MANULA KILA WAKICHEZA NA SIMBA…

Habari za Simba

Mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube amefichua siri ya kuifungia timu yake bao la mapema dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Dube alifunga bao hilo dakika ya kwanza tu ya mchezo ikiwa ni bao lake la sita kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu na la pili kuifunga Simba baada ya mechi ya kwanza Oktoba 27, mwaka jana kuipatia timu yake ushindi wa 1-0.

“Siri kubwa ni maandalizi na ushirikiano uliopo baina yetu wachezaji, mchezaji mkubwa hachagui sehemu ya kufanyia mambo makubwa hivyo kwangu ni furaha kuisaidia timu yangu japo tumekosa pointi tatu,” alisema.

Dube aliongeza kwa jinsi ambavyo walivyocheza walistahili kupata ushindi ingawa kitendo cha kutokupoteza kwao pia ni kizuri.

“Tulianza mchezo vizuri na kipindi cha pili tulicheza kwa tahadhari kubwa ya kulinda ushindi wetu ingawa makosa tu madogomadogo na kukosa umakini dakika za mwisho zikatufanya kupoteza pointi mbili zaidi,” alisema Dube.

Mbali na Dube kufunga bao hilo ila mastaa wengine waliofunga mabao ya mapema ni aliyekuwa beki wa Mtibwa Sugar, Nickson Kibabage (dakika ya kwanza) dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare ya 2-2 Oktoba 2, mwaka jana.

Ismail Mgunda wa Tanzania Prisons aliifungia timu yake bao dakika ya pili tu kwa mkwaju wa penalti wakati iliposhinda mabao 2-1 na Dodoma Jiji, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Liti Singida.

Salum Kipemba wa Polisi Tanzania alifunga bao dakika ya pili pia wakati timu yake ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya KMC Agosti 21, mwaka jana huku Moses Phiri wa Simba akifunga bao la dakika ya tatu dhidi ya KMC katika sare ya 2-2 Septemba 7, mwaka jana.

SOMA NA HII  KWA HALI JINSI ILIVYO...YANGA WAKIZUBAA KIDOGO TU ..IMEKULA KWAO MAZIMA...ISHU IKO HIVI 'MWAMBA'...