Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KUHUSU HALI YA SIMBA GUINEA NA WALIVYOPOKELEWA UWANJA WA...

HUU HAPA UKWELI KUHUSU HALI YA SIMBA GUINEA NA WALIVYOPOKELEWA UWANJA WA NDEGE..

Habari za Simba SC

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kikosi hicho kimewasili salama nchini Guinea juzi saa 11 jioni na kila kitu kinakwenda sawa kuelekea mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya.

Ahmed amesema hali ya hewa ya Mji wa Conakry ambapo mchezo wetu utafanyika ni sawa na jijini Dar es Salaam hivyo wachezaji hawatapata changamoto yoyote inayohusiana na hali ya hewa.

Ahmed ameongeza kuwa kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho jana jioni katika uwanja wa (Stade General Lansana Conte)ambao utatumika kwenye mchezo wa leo.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumefika salama nchini Guinea juzi jioni. Wachezaji walipewa mapumziko na wamefanya mazoezi ya mwisho jana jioni kabla ya leo kushuka uwanjani.

“Kwa kweli hatukupata changamoto yoyote ya nje ya uwanja, baada ya kufika usafiri ulikuwepo tayari kutupeleka hadi hotelini tulipofikia kwa hiyo hali ni nzuri,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  JEZI YA MTANZANIA YAUZWA UBELGIJI