Home Habari za michezo MASIKINI MWAKINYO WEEHH…AZIDI KUPOROMOKA KWENYE VIWANGO VYA MABONDIA DUNIANI…

MASIKINI MWAKINYO WEEHH…AZIDI KUPOROMOKA KWENYE VIWANGO VYA MABONDIA DUNIANI…

Hassan Mwakinyo

Wakati Hassan Mwakinyo akiendelea kuporomoka duniani, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imesema, Mwakinyo na menejimenti wanajukumu la kupindua meza.

Mtandao wa ngumi za kulipwa wa Dunia (Boxrec) umemtaja Mwakinyo kuwa ni bondia wa 64 kati ya mabondia 1,920 akiporomoka mara mbili zaidi japo ameendelea kusalia namba moja nchini kati ya mabondia 32 wa uzani wa super welter akiwa na nyota tatu.

Mwaka 2018, Mwakinyo alipanda hadi nafasi ya 14 akiwa na nyota nne baada ya kumchapa Sam Egginton ambaye aliporomoka kwenye ubora ingawa sasa Boxrec inamtaja ni wa 18 duniani na wa pili Uingereza akiwa na nyota nne huku Mwakinyo akizidi kuporomoka kutoka nafasi ya 37 aliyokuwepo wiki kadhaa zilizopita hadi wa 64.

“Kiutaratibu bondia asipopigana, wale wanaocheza wanapanda na yeye anaporomoka na ikifika mwaka mmoja bila kucheza maana yake anakuwa inactive ndicho kinatokea sasa kwa Mwakinyo,” alisema rais wa TPBRC, Chaurembo Palasa.

“Kwa Mwakinyo sisi hatuwezi kumlazimisha kucheza au kumtafutia pambano, huo ni utaratibu wake na menejimenti yake, hata hivyo yeye ni bondia mkubwa na ana mipango yake, anajua mipango yote ya kurudi kwenye renki za juu, TPBRC kazi yetu ni kusimamia tu, utakapofika wakati atapigana na atarudi kwenye ubora, hiyo ni mipango yake.

Mwakinyo tangu Sepotemba 3, mwaka jana alipochapwa na Liam Smith kwa Technical Knock Out (TKO) nchini Uingereza, hajarudi ulingoni hadi sasa huku pambano lake la Zanzibar mwanzoni mwa mwaka huu likigonga mwamba licha ya karibuni promota wake, Shomari Kimbau kueleza litachezwa Aprili.

Bondia huyo aliyeondoshwa kileleni kwenye ubora wa kila uzani ‘pound for pound’ ya Tanzania aliyokuwa aikiishilia zaidi ya miaka mitatu aliwahi kuingia kwenye 20 bora ya dunia alipomchapa Eggington kwa TKO mwaka 2018 nchini Uingereza na kuwa wa 14.

Tangu wakati huo amekuwa kwenye panda shuka katika mapambano mapambano manane aliyopigana baada ya lile la Eggington huku sita yakiwa ni ya kimataifa na kushinda yote kabla ya kuchapwa na Smith mwaka jana.

Aliyewahi kuwa promota wa bondia huyo, Ally Mwazoa alisema kwa levo aliyofikia Mwakinyo kupata promota wa kumuandalia pambano nchini ndiyo kikwazo.

SOMA NA HII  ATAKALO MUNGU HAKUNA WAKUPINGA...MANENO YA 'SHOMBO' YAMPA 'MANDONGA' ULAJI YANGA...ALAMBA SHAVU HILI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here