Home Habari za michezo RASMI…BAADA YA KUCHOSHWA NA TABIA ZAKE..NABI AMPIGA CHINI MAZIMA MORRISON…ISHU IKO HIVI…

RASMI…BAADA YA KUCHOSHWA NA TABIA ZAKE..NABI AMPIGA CHINI MAZIMA MORRISON…ISHU IKO HIVI…

Habari za Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema uwezekano wa winga wake Bernard Morrison kusafiri na wenzake kwenda Tunisia kuwafuata wapinzani wao US Monastir ni mdogo sana kutokana na kile alichokisema ameumia.

Nabi alisema Morrison aliumia akiwa kwao Ghana na kwamba atakuwa nje kwa muda mrefu, lakini akawashusha presha mashabiki wa timu hiyo kuwa Yanga itaendelea na maisha kama kawaida.

“Sioni uwezekano wa Morrison kusafiri na timu, nafikiri huyo ndio mchezaji tunayeweza kumkosa katika safari hii lakini nimekueleza kuwa nafasi yake itazibwa,” alisema Nabi na kuongeza;

“Kuna mpango tumeshaanza kuufanyia kazi jinsi ya kutafuta mtu muafaka wa kuziba nafasi yake na anaweza kuwasapraizi watu siku ya mchezo wetu wa kule.”

SOMA NA HII  BENCHIKHA:- KWA SIMBA HIII BADO SANA...NDIO KWANZAAAA ASILIMIA 70 TU YA NAVYOTAKA IWE...