Home Habari za michezo SAKATA LA FEI TOTO KURUDI YANGA…INJINIA HERSI AVUNJA UKIMYA…AANIKA WANAOMRUBUNI ILI ASIRUDI...

SAKATA LA FEI TOTO KURUDI YANGA…INJINIA HERSI AVUNJA UKIMYA…AANIKA WANAOMRUBUNI ILI ASIRUDI KAMBINI…

Tetesi za Usajili Yanga

Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said amesema mpaka sasa mchezaji wa klabu hiyo Feisal Salum hajaripoti kambini kuendelea na majukumu yake hivyo kama klabu bado inaendelea kumkumbusha kuwa anatakiwa kurudi kambini hapo.

Akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Clouds 360, Eng. Hersi amesema matakwa ya kimkataba yanamhitaji mchezaji huyo ili kulipa stahiki zake katika kipindi chote ambacho hakuwepo.

“Sisi Feisal ni mchezaji wetu, ni kijana wetu. Suala hili linaloendelea kuna watu wanaweza kuwa wanaongeza chumvi nyingi huko kwenye mitandao, sisi kwetu hicho kitu siyo muhimu tuna mkataba na mchezaji mpaka 2024,” ameeleza.

Aidha, amesema kama kuna mtu ambaye anamlaghai mchezaji huyo anapaswa kupigwa vita kwa kuwa kuna utaratibu wa kufuata ikiwa mchezaji atahitajika na si kupita nyuma ya pazia.

Hata hivyo ameeleza kuwa endapo mchezaji huyo ataamua kurudi kambini, atapokelewa kwa mikono miwili na kupewa sapoti yote ili kutimiza majukumu yake kama mchezaji.

Aidha, Hersi amesema kuwa Yanga imeandika barua kuomba siku ya kusikilizwa kwa mapitio ya shauri la mkataba wa Feisal Salum kusogezwa mbele kwa kuwa Februari 27, 2023 iliyopangwa, viongozi watakuwa nje ya nchi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Real Bamako ya Mali.

Hersi ameongeza kuwa wao kama klabu wanaendelea kutimiza wajibu wao kwa mchezaji wao ikiwa ni pamoja na kumlipa mshahara na stahiki zake kama kawaida mchezaji huyo licha ya kutokuwepo kamibini.

“Mchezaji aliomba marejeo (Review) ya maamuzi hayo ambayo yalimepangwa kusikilizwa Februari 27, 2023, tumeandika barua kwenda kwenye Kamati kuomba shauri hilo lisogezwe mbele kwa kuwa tunatarajia kuwa na mechi Februari 26 nchini Mali.”

Kuhusu kama Yanga bado inamhitaji Fei? “Hapo kuna mambo mawili, mkataba ni ishu ya taasisi na ni suala la mkataba, Fei ana mkataba na anatakiwa kurudi, kuhusu suala binafsi sisi Fei ni kijana wetu, kuna watu wanaongeza chumvi, ni mchezaji wetu na ataendelea kuwa kwetu hadi Mwaka 2024.”

Kama Fei alishawishiwa je? “Kama Feisal atakuwa ameshawishiwa na mtu, huyo mtu anatakiwa kupigwa vita, soka ina njia zake za kupita, kwa nini uanze kupitia njia ambazo si sahihi, siwezi kumlaumu Fei kama ivyo ndivyo, lakini tunatakiwa kufuata njia.”

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA SC WALA KIAPO KUMALIZIA KAZI YA DAR...HISTORIA KURUDIWA..?

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here