Home Burudani ACHANA NA RONALDO…HUU HAPA MCHUMA ANAOTUMIA MESSI KUPAA NAO ANGANI…NI NOMAA NA...

ACHANA NA RONALDO…HUU HAPA MCHUMA ANAOTUMIA MESSI KUPAA NAO ANGANI…NI NOMAA NA NUSU…

Ndege ya Messi

Hii ndio Ndege binafsi anayotumia Nyota wa Argentina Lionel Messi inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani milioni 15.

Ndege hiyo ya kifahari ina majina ya familia kwenye ngazi yani Leo, mkewe Antonela na watoto wao Thiago, Ciro na Mateo. Vilevile ina nambari 10 mkiani, namba ambayo imekuwa alama kwa nyota huyo ikiwa ni namba aliyoitumia kwa muda mrefu wakati akiichezea FC Barcelona.

Ndani yake kuna jiko, mabafu mawili na viti vya kutosha watu 16.Viti hivyo vinaweza kukunjwa na kugeuka kuwa vitanda 8.

Ndege hii haimilikiwi na Messi bali ameikodisha na anaitumia yeye tu, hivyo haikodishwi kwa mtu mwingine yoyote kwa sasa.

Usafiri huu wa haraka unamsaidia sana nyota huyo ukizingatia ratiba zake ngumu ambapo anatakiwa kuwepo sehemu tofauti duniani mara kwa mara kuhudhuria hafla mbalimbali, kucheza soka na kufanya kazi za chapa kadhaa anazoziwakilisha.

Isitoshe inamuwezesha kusafiri na familia yake pamoja na marafiki kwenye mapumziko.

SOMA NA HII  ISHU YA MORRISON KUZUIWA KUINGIA SAUZI..MASHABIKI WA SIMBA SAUZI WAIBUKA NA HILI..WATOA ONYO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here