Home Azam FC AZAM FC NDIO BASI TENA…KOCHA AWASHANGAA MASTAA WAKE…WAJITOA WENYEWE

AZAM FC NDIO BASI TENA…KOCHA AWASHANGAA MASTAA WAKE…WAJITOA WENYEWE

AZAM FC NDIO BASI TENA...KOCHA AWASHANGAA MASTAA WAKE...WAJITOA WENYEWE
KALI ONGALA KOCHA WA AZAM FC

Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala, amefunguka kuwa anasikitishwa na mwenendo wa timu hivyo kwa kushirikiana na
benchi la ufundi watahakikisha kuwa wanafanya maboresho ili hali hii isijirudie tena.

Matumaini ya Azam FC kutwaa ubingwa kwa msimu wa 2022/23 yalizimwa na Ihefu baada ya (Machi 12) kuwatungua bao 1-0 Uwanja wa Highland Estate, Mbeya.

Kichapo hicho kinaifanya Azam FC kusalia na pointi zake 47 baada ya kucheza mechi 25 wamebakiwa na mechi tano ambazo ni pointi 15 ambazo hata ikitokea wakashinda zote hawatawakuta vinara Yanga wenye pointi 65.

Akizungumza nasi, Ongala alisema: “Inasikitisha sana kuona wachezaji wangu wakicheza kwa hali ya chini kiasi hiki hasa katika mechi za ugenini ambazo tumekuwa tukipoteza zaidi.

Ligi inasimama kupisha michuano ya kitaifa na kwa upande wetu sisi hatutopumzika, tutakuwa mazoezini kuhakikisha kuwa tunafuta kila aina ya matatizo ambayo yamejitokeza kwenye mechi zetu zilizopita na hatutopumzika hadi ligi itakaporejea.

“Tukirejea tena kwenye ligi kila mechi tutakayocheza kuanzia Coastal Union na zengine zilizobaki tutakua tunakusanya alama tatu tu mpaka ligi iishe.”

SOMA NA HII  SURE BOY, HIMID MAO WARUDI TAIFA STARS....BOCCO, KASEJA WATUPIWA VIRAGO TIMU YA TAIFA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here