Home Habari za michezo BEKI WA SIMBA SHOMARI KAPOMBE “MECHI NA RAJA CASABLANCA…NI MAZOEZI TU

BEKI WA SIMBA SHOMARI KAPOMBE “MECHI NA RAJA CASABLANCA…NI MAZOEZI TU

BEKI WA SIMBA SHOMARI KAPOMBE

BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema mchezo wa
marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa Aprili 1, 2023 nchini Morocco utakuwa na faida mara mbili.

Mlinzi huyo wa kulia, Kapombe amedai kwakuwa tayari
wameshafuzu hatua ya Robo Fainali hivyo watautumia mchezo huo na Raja CA kama sehemu ya maandalizi kuelekea hatua inayofuata.

“Mchezo utakuwa mgumu, Raja ni timu kubwa Afrika na tunaenda kwao. Tayari tumefanikiwa kutinga robo fainali hivyo tutautumia mchezo dhidi ya Raja kama sehemu ya maandalizi sababu ni mechi ya mwisho ya kundi,” amesema Kapombe.

SOMA NA HII  RIVERS UNITED WAZIDIWA KETE NA YANGA...WACHACHAWA! WAPAGAWA!...ISHU NZIMA IKO HIVI