Home Ligi Kuu BIASHARA UNITED YASHINDWA KUJIENDESHA…WALIPIWA MADENI ZAIDI YA MIL 39…TIMU KUBADILISHWA JINA

BIASHARA UNITED YASHINDWA KUJIENDESHA…WALIPIWA MADENI ZAIDI YA MIL 39…TIMU KUBADILISHWA JINA

BIASHARA UNITED YASHINDWA KUJIENDESHA...WALIPIWA MADENI ZAIDI YA MIL 39...TIMU KUBADILISHWA JINA

ULIOKUWA uongozi wa mpito wa Biashara United umekanusha taarifa za timu hiyo kuuzwa huku ukiweka wazi kilichofanyika ni kuwakabidhi wadau kuiendesha baada ya wao kushindwa kutokana na ukata.

Akizungumza na Mwanaspoti aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo kwa kipindi cha mpito, Augustine Mgendi alisema Biashara haikuuzwa bali imekabidhiwa kwenye kampuni ya Free Sports Limited kupitia mkutano mkuu wa dharura wa wanachama.

“Kwanza walionyesha dalili na mapenzi mema kwa timu kwa kulipa posho na usafiri kwenye mechi za African Sports na Mbuni hivyo tukaamua kuwakabidhi kwa muda usiojulikana kuiendesha timu hiyo na kama watashindwa wanapaswa kuirejesha ofisi ya Mkoa wa Mara.

“Tulikubaliana pia walipe madeni ya wanachama waliojitolea takribani Sh39 milioni, lakini wakatupa tena Sh10 milioni na kulipa madeni mengine madogo madogo ingawa watabadili jina na kuitwa Mara United,” alisema Mgendi.

Mgendi aliongeza kuendesha timu inahitaji nguvu ya kifedha na wanaamini uwezo wa kampuni hiyo utasaidia kuirudisha Ligi Kuu kwa msimu wa 2023/24 baada ya msimu huu hesabu kukwama.

Licha ya kampuni hiyo kukabidhiwa timu, haitaruhusiwa kuihamisha kutoka mkoani Mara wala kuiuza pale itakaposhindwa kuiendesha kwa siku za usoni.

SOMA NA HII  BANGALA AMKINGIA KIFUA FEI TOTO