Home Taifa Stars KAKOLANYA AFURAHIA KUITWA STARS…KUJIWEKA SAWA MUDA WOTE NI MUHIMU…HATA NIKIKAA BENCHI FRESH...

KAKOLANYA AFURAHIA KUITWA STARS…KUJIWEKA SAWA MUDA WOTE NI MUHIMU…HATA NIKIKAA BENCHI FRESH TU

KAKOLANYA AFURAHIA KUITWA STARS...KUJIWEKA SAWA MUDA WOTE NI MUHIMU...HATA NIKIKAA BENCHI FRESH TU

Kipa wa Simba, Beno Kakolanya amesema japokuwa anapata nafasi ndogo ya kucheza ndani ya kikosi, lakini kuitwa Taifa Stars kunampa nguvu ya kupambana.

Kalolanya ni mmoja kati ya wachezaji 31 walioitwa Taifa Stars ambayo itaingia kambini kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika dhidi ya Uganda utakaopigwa Machi 24.

Wakati anazungumza Beno alisema inapotokea nafasi ya kucheza humfanya aitumie vyema ili kuonyesha kipaji, jambo linalompa faraja kwani kazi yake inathaminiwa hadi kuonekana Stars.

“Kuna makipa wengi Tanzania, lakini kocha kuona nafaa kuwa miongoni mwa kikosi chake imeniongezea morali ya kazi nikijua ipo siku hadi kwenye kikosi changu nitakuwa chaguo la kwanza,” alisema.

Beno ambaye tangu ajiunge Simba amekuwa namba mbili nyuma ya Aishi Manula aliyeitwa naye Stars, na alisema anapenda ushindani unaomfanya kulinda kiwango chake, akiamini siku akihitajika kwenye majukumu awe tayari kuibeba timu.

“Nimejifunza kujiweka tayari muda wote kwa ajili ya majukumu yangu bila kujali nacheza ama sichezi, kwani najua ilimradi nikiwa kwenye timu kuna siku nitahitaji kufanya kazi,” alisema.

“Nikiwa benchi, nikicheza yapo mengi ninayojifunza kiufundi yanayonifanya niendelee kuboresha kipaji changU. alisema kakolanya

SOMA NA HII  HILI HAPA JESHI LA STARS DHIDI YA NAMIBIA LEO USIKU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here