Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA VIPERS…MBRAZILI ABADILI ‘GIA ANGANI’ SIMBA….AINGIZA MBINU ZA KIMAFIA…

KUELEKEA MECHI NA VIPERS…MBRAZILI ABADILI ‘GIA ANGANI’ SIMBA….AINGIZA MBINU ZA KIMAFIA…

Habari za Simba SC

Baada ya Simba kuichapa Vipers bao 1-0 ugenini Uganda wikiendi iliyopita na kupewa mapumziko ya siku moja,  Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amekuja na mpango kazi mpya wa mabao wa kuongeza idadi ya mabao kwani ameshtukia kitu.

Hiyo ni baada ya Simba kuonekana kupunguza kasi ya kupachika mabao, ikiwa imefunga mawili tu katika mechi nne zilizopita, tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika na moja dhidi ya Azam iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 ambalo hata hivyo ni la kujifunga kwa beki Abdallah Sebo hivyo kiuhalisia wachezaji wa Simba katika mechi nne za mwisho wamefunga bao moja tu.

Simba imekuwa ikitengeneza baadhi ya nafasi lakini washambuliaji wake wakiongozwa na nahodha John Bocco, Jean Baleke, Habib Kyombo na Moses Phiri kushindwa kuzitumia katika nyakati tofauti jambo lililogunduliwa na benchi la ufundi la chama hilo na kueleza mabadiliko makubwa yanaenda kufanyika.

Kocha Robertinho amesema kuwa, vipaumbele vyake ni timu icheze vizuri, kwa kasi na ipate ushindi lakini pia anafurahi ikishinda mabao mengi huku akigusia michuano ya CAF ambayo anaamini mabao yana faida zaidi.

“Pamoja na ushindi ugenini lakini bado tuna tatizo katika eneo la mwisho. Baadhi ya nafasi tunazotengeneza zinapotea hilo linamuumiza kila mtu kati yetu na tunaenda kulifanyia kazi licha ya kwamba tumeshajua wapi tunaanzia,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Katika mashindano yote tuliyopo tunahitaji mabao, hususani haya ya CAF ndio tunahitaji kufunga zaidi kwani inaweza kufika sehemu mkalingana alama na mwenzako na kitakachoamua kikawa mabao.

“Hivyo lazima tufanye kazi juu ya hilo, wachezaji wote kwa pamoja tutawaeleza mahitaji yetu na faida za kupata mabao na mwisho tutaenda kwenye uwanja wa mazoezi kutekeleza hilo kwa vitendo,”alisisitiza.

Simba iliibuka na ushindi wa goli 4-0 dhidi  African Sports jana Alhamisi  kwenye mechi ya FA na baada ya hapo itarudiana na Vipers Machi 8 kwa Mkapa kisha itaivaa Mtibwa Sugar kwenye Ligi Kuu Machi 11, 2022.

Robertinho hadi sasa ameiongoza Simba kwenye mechi saba, tatu za Ligi Kuu na tatu za Ligi ya Mabingwa Afrika  pamoja na moja ya FA na kufunga jumla ya mabao kumi ambayo ni wastani wa bao moja na nusu kwa kila mechi.

Mabao hayo ni 4-0 dhidi ya African Sports, 3-2 dhidi ya Mbeya City, 1-0 mbele ya Dodoma, na sare ya 1-1 na Azam huku kimataifa likiwa lile moja na la ushindi mbele ya Vipers.

SOMA NA HII  MUKOKO ATINGISHA KIBERITI YANGA...ATOA SHARTI LA MKATABA MPYA..AGUSIA ISHU YA KUJIUNGA SIMBA...