Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA VIPERS…SAMATTA AWAPA UJANJA SIMBA…MBRAZILI KUIBUKA NA MBINU ZA KIMAFIA…

KUELEKEA MECHI NA VIPERS…SAMATTA AWAPA UJANJA SIMBA…MBRAZILI KUIBUKA NA MBINU ZA KIMAFIA…

Habari za Simba

Simba wikiendi iliyopita ilifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers ya Uganda kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa St Mary’s nchini humo, huku Kocha Oliviera Robertinho akiwaonya mabosi wake.

Huu ulikuwa mchezo wa tatu kwa Simba kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu baada ya awali kupoteza dhidi ya Horoya ugenini na Raja Casablanca kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Katika kundi la Simba ipo nafasi ya tatu na pointi tatu nyuma ya vinara Raja wenye pointi tisa na Horoya wenye pointi nne na sasa inatarajiwa kuikaribisha Vipers kwenye mchezo wa nne jijini Dar es Salaam.

Kikizungumza chanzo cha ndani ya Simba, kinasema kocha wa timu hiyo ameshatoa tahadhari ya mchezo ujao utakaopigwa wiki ijayo na uongozi wa timu umeshaanza kuchukua tahadhari.

Kocha huyo amewaeleza mambo mengi ambayo waliyafanya walipokuwa wanavaana na TP Mazembe kwenye mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutinga hatua ya makundi na kusema kuwa ndiyo vitu ambavyo viliwasaidia sana kupata ushindi.

“Baada ya mchezo kumalizika Robertinho alitoa tahadhari kubwa sana kwa Vipers kila wanapokwenda ugenini kucheza na mpinzani wao kuwa wanajiandaa vizuri zaidi ndani na nje ya uwanja kufahamu mpinzani anafanya nini kwa wakati husika.

“Alitoa mifano mingi jinsi ambavyo walifanya wakati wanakwenda kuvaana na Mazembe nchini Congo mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu na kusema jamaa huwa wanajiandaa mara mbili ya jinsi ambavyo wanafanya wakiwa nyumbani kwao.

“Alisema kwanza huwa wanakuwa na mashushushu kila sehemu na wana uwezo mkubwa sana wa kupata mbinu za wapinzani wao wanafanya nini kwao na wanajiandaa vipi, pia alitushauri tuhakikishe kuna mtu anabaki pale Uganda au anaenda kuhakikisha pia anatupa taarifa za jamaa wanafanya nini kwa kuwa anasema wanabadilika kila wakati na bosi wao hapendi kupoteza mchezo hata kama utakuwa wa kirafiki na hata ule waliowafunga Yanga mabao 2-0 siku ya Mwananchi yalikuwa ni maagizo lazima washinde.

Hata hivyo, chanzo hicho kilisema Simba wameshafanya kila jambo kuhakikisha kuwa wanapata ushindi kwenye mchezo huo huku pia wakiwa wanaendelea kupata kila kitu ambacho Vipers wanafanya kutoka kwa watu ambao wapo pale Uganda.

“Tofauti na mechi nyingi hii ni muhimu zaidi, kuna kikao nafikiri ni kila siku jioni na yote ni kuhakikisha kuwa tunafahamu tupo wapi na tunakwenda wapi ili tuweze kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao utatupa dira ya kwenda hatua ya makundi, ukweli yale yaliyotokea dhidi ya Raja hayatakiwi kujirudi na tunarekebisha makosa ya wapi tulikosea,” kilisema Chanzo hicho.wadau watoa neno.

Mchezaji wa zamani wa Simba, Ally Pazi Samatta alisema ili mastaa wa kikosi hicho wapate ushindi dhidi ya Vipers ya Uganda wakiwa nyumbani, watahitaji kutengeneza nafasi nyingi na kuhakikisha wanazitumia kwa umakini.

Mzee huyo ambaye ni baba mzazi wa Mbwana Samatta anayecheza kwa mkopo Genk, alisema;

“Simba inatakiwa iandae wachezaji kiakili kujua licha ya kushinda ugenini wapinzani wao wanahitaji pointi tatu, hilo litawafanya waongeze nidhamu na bidii ya kuhitaji kusonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo Uganda.”

Kwa upande wa Emmanuel Gabriel staa wa zamani wa kikosi hicho, alisema safu ya ushambuliaji iongeze umakini wa kutengeneza nafasi na ulinzi uimalishwe ili kupata ushindi dhidi ya Vipers, mchezo wa marudiano.

“Kitu ambacho mastaa wa Simba wanatakiwa waweke umakini wasiikariri kiwango ambacho Vipers ilikionyesha kwao, badala yake wajue mchezo unaweza ukabadilika, hivyo wajipange kwa ushindani zaidi na waheshimu wapinzani wao,” alisema.

SOMA NA HII  AHMED ALLY:- SIMBA HAKUNA UBOVU HUO KIVIILEE ...AL AHLY WALITUWAHI TU....